Kwa kweli nimesikitishwa sana namna chama mahiri cha upinzani kama CDM kudhalilika kiasi hiki katika uchaguzi huu mkuu. Niliipenda CDM-Asilia lakini ilipoingiliwa na wana CDM-Maslahi niliamua kuitosa na kumpigia debe Magufuli.
Uchaguzi umekwisha na tunae Raisi.
Je Tunao Upinzani Mahiri Tena?
Kwa kweli CDM imeathirika sana na inaweza kumeguka vipande vipande. Kwa sasa naona ACT-Wazalendo wanaweza kupata wafuasi wengi sana na kuwa chama kikuu cha upinzani ifikapo 2020. Sidhani kama tuna upinzani mahiri tena kwa sasa.
CDM Wafanye Nini Sasa:
Cha kwanza ni kumng'oa haraka sana yule rubani aliebadilisha gia angani na kukiangamiza CHOMBO.
YES, lazima mheshimiwa Mbowe awajibike haraka sana kama wana CDM watakuwa na imani tena na chama chao, la sivyo itakuwa ni mafuriko kuelekea ACT, au CCM. Leadership ethics zinamshinikiza Mbowe aachie kiti.
Utabiri wangu uchwara ni kuwa sidhani CDM inaweza kuji-rehabilitate tena katika miaka mitano ijayo. Pengine ni mpaka 2025 ndio wanaweza kuwa na nafasi ya kuwania uraisi ikiwa tu mabadiliko katika ngazi za juu yawe yalishafanyika jana.
Katika mabadiliko haya ya ngazi za juu ni muhimu CDM wasiwape waTanzania hisia ya kuwa hiki ni chama cha watu wa kanda ya kaskazini - itawagharimu sana.
Tanzania haiwezi kusonga mbele kama chama tawala hakiwezi kuogopa kuwa kuna upinzani mahiri. Kwa anguko hili la CDM na UKAWA, Tanzania hakuna upinzani tena, trust me.
Sheikh Mbowe mdogo wangu, kiongozi wangu, jipime halafu ukinusuru chama. Bado muda upo lakini hii window of opportunity ni fupi sana.
source - jamii forums
Post a Comment