BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imehairisha kesi namba 37 ya mwaka huu, ya
mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha
(1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa
mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo. Anaandika Josephat Isango …
Jopo hilo la majaji linaongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo pamoja na Lugano
Mwandambo na Aloysius Mjujulizi limeahirisha kesi ya kikatiba
iliyofunguliwa na mgombea ubunge Viti Maalum kupitia Chadema, Ammy
Kibatala.
Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa
serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka
pingamizi sababu walipokea notisi ya walalamikaji muda wa jioni hivyo
hawakujiandaa.
“Mheshimiwa Jaji, tunaomba tupewe muda kwani tulipokea nyaraka hizi muda
wa kazi ukiwa umekaribia kwisha hivyo hatukujiandaa, tunaomba tupewe
muda kama ikiwezekana tulete majibu saa 8:30 Mchana leo kama mahakama
itaona inapendeza,” alisema Wakili wa Serikali Obadia Kameya.
Kabla Majaji hawajatolea uamuzi ombi hilo walimshauri Wakili wa
mlalamikaji, Peter Kibatala kubadilisha mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi
wa Uchaguzi kwani ndiye mtendaji mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuangalia katiba Ibara ya 74, kifungu
kidogo cha 7, inayosomeka “Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu
yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara
huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa
majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa
Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya
sheria iliyotungwa na Bunge.”
Baada ya marekebisho hayo, kesi hiyo iliyovutia watu wengi iliahirishwa mpaka kesho saa 3
Mawakili upande wa mlalamikaji ni Peter Kibatala na Omary Msemwa, huku
upande wa walalamikiwa ambayo ni Mwanasheria Mkuu na Tume ya Uchaguzi ni
Obadia Kameya na Alecia Mbuya.
Katika kesi hiyo, mgombea huyo ambaye pia ni mpiga kura mwenye maslahi
na uchaguzi mkuu ujao, ameomba mahakama kwa mujibu wa kifungu hicho sura
ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ifafanue kuhusu haki za
wapiga kura.
Mlalamikaji anaitaka mahakama iseme na kutafsiri kifungu hicho
kinamaanisha nini kuhusu haki hiyo kufuatia kauli iliyotolewa na NEC
pamoja na Rais Jakaya Kikwete kwamba wananchi wakishapiga kura
hawaruhusiwi kukaa eneo la vituo vya kupigia kura umbali wa mita 200.
Aidha, anaitaka mahakama itamke kama ni halali kwa Rais na Tume ya
Uchaguzi (NEC) kuzuia wananchi kukaa kwa utulivu umbali huo ama la.
MWANAHALISI ONLINE
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...



Post a Comment