Na Happiness Katabazi
LEO Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika
Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana
hongereni sana.
Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi
huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.Nimewasikia wote
waliopewa nafasi ya kuzungumza a amezungumza waliyozungumza hata Waziri
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote
aliyoyasema Sumaye siyo mapya.
Lakini wenye akili timamu
tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye amewahi
kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.
Enzi akiwa Waziri Mkuu wa
serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO
ZIKUNYOKEE VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii
ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.
Nirudi Kwenye mada yangu ya
Msingi ya Leo.Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA
kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa Leo saa 11 jioni alipopanda
jukwaani kuanza kuhutubia alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni
hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi
kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.
Kwasababu hiyo eti Mbowe na
viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo
hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.
Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania.
Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya
Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja Uwanjani kueleza wanachi
atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .
Lakini Lowassa Hilo Leo lime
mshinda kashindwa kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya
serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu
kabisa.
Mgombea urais kabisa bila aibu
Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti
hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website?
Tumuulize huyu Lowassa ambaye
amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa
tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .
Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website?
Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi
hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye
simu hawana uhakika wa kuzipata.
Sasa ikitokea wasikupigie kura za
Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako
utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?
Maana hata unapotaka Mwanamke
kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au
aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi
wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?
Kama Mbowe na viongozi wenzake
walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili
upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?
Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako?
Kama ulishauriana na viongozi wa
UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya
mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.
Hilo limekushida,Je ikitokea
ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata
nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma
hotuba au mhadhara kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?
Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa
vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia
kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?
Polisi wakikukataza kisheria
kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu
Katika Jamii ndiyo wanakuchukia?
Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.
Leo umetumia dakika nane jukwaani
kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la
kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye eti
amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.
Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.
Na pia nimeliona jipya pia kwa
mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi
wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa
wanakupiga vijembe.
Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki mna misimamo inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?
Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.
Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa
Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa
Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.
Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo
kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana
wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake
wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani
walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.
Yaani mgombea Urais kabisa wa
UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais
Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO
Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza
hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?
Lowassa Leo Kasema anajua tu
ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini
unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema
utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani
na kwasababu gani?
Msimnajipata Kuwa UKAWA
mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama
mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe
kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?
Hivi Lowassa kwa usanii huu
unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika
kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu
huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa
na usanii wa wazi kabisa.
Lowassa jiulize kwanini Hilo
limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka
kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia kutoka kwako
hawajalipata maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.
Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya
Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa
hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa
kisingizio cha muda kumalizika.
Je hatuoni hii ni mbinu
iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba
hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.
Mungu ibariki Tanzania
0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
29/8/2015
Post a Comment