Leo mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba ameita waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam. Tuwe pamoja kujulishana kitachojiri makuu ya chama, Buguruni baada ya muda si mrefu.
=====

Sakaya: Majadiliano yamechukua muda mrefu kuliko tulivyodhani, tunaomba radhi kwa kuchelewa na tunaahirisha press conference ya leo.

Kuna majadiliano kati ya wazee na mwenyekiti wa chama na yakikamilika na ikaonekana bado kuna haja ya kuwaita waandishi, mtaitwa.

Itakuwa ni kupiga ramli kutabiri, mwenyekiti atakuja kuongea mwenyewe, Yaliyopo kwenye social networks ni mambo..
=======

Kuna mwandishi alipigwa na feni baada ya kusimama juu ya meza, wakati waandishi wanamuhudumia, meza ikaahirisha kikao.

Kuna wanachama wengi nje ya makao makuu wakisema wana imani na Lipumba, wanaimba nyimbo kadhaa.
=======

Lipumba amekanusha uvumi wa kuondoka CUF na amesema yapo mambo mengi ya kuendelea kuyatafakari ndani ya chama cha CUF kwa sababu CUF ni taasisi kubwa na sio ya maamuzi ya mtu mmoja, mwenyekiti hakuruhusu kuulizwa maswali.