Zipo taarifa za uhakika kwamba Edward Lowasa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu
kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond anatarajia kuzungumza na waandishi wa
habari Jumapili tarehe 26 Julai 2015 Jijini Dar es Salaam. Katika
mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kueleza mambo mengi juu ya mchakato wa
uchaguzi ndani ya CCM uliopelekea jina lake kukatwa.
Pia katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kutangaza rasmi kujivua
uanachama wake ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ambapo baadaye jioni
ataelekea viwanja vya Mwembeyanga ambako ataungana na viongozi wengine
wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadharaza. Mtakumbuka kuwa uwanja huo wa
Mwembeyanga uliopo Temeke Dar es Salaam ulitumika kutaja orodha ya
mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa mwaka 2007 ambapo
jina la Lowasa lilikuwa miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha hiyo.
Uamuzi wa Lowasa kwenda CHADEMA umetokana na kutimiza makubaliano ya
kupeleka shilingi bilioni 10 ambapo fedha hizo zimekabidhiwa Jana
Alhamis Tarehe 23 Julai 2015. Aliyekabidhi fedha hizo kwa Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe ni Apson Mwang'onda na makabidhiano yamefanyika
kwenye Hotel ya Sea Cliff huku tukio hilo likishuhudiwa na Kingunge
Ngombale Mwiru na wengine ambao sitawataja kutokana na sababu maalum.
Taarifa zinasema kuwa kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa watu
walioathirika na kukatwa kwa Lowasa hasa kutokana na fedha nyingi na
muda kwa matumaini kuwa watakuwa "UPPER" baada ya Lowasa kushinda Urais.
Miongoni mwao ni pamoja na Prof Juma Kapuya, Nazir Karamagi, Parseko
Kone, Mgana Msindai, Kingunge Ngombale Mwiru, Mchungaji Gwajima, Andrew
Chenge nk.
Post a Comment