BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian
Lubuva, amesema kura zote za urais, ubunge na udiwani, zitahesabiwa
katika vituo vya kupigia kura na matokeo yote kutangazwa hapo hapo na ni
marufuku kusafirisha masanduku ya kura kama ilivyokuwa zamani.
Jaji Lubuva aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano na
wawakilishi wa walemavu kujadili namna bora ya wao kushiriki katika
Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu ni marufuku kuhamisha masanduku ya
kura kwa sababu vituo vya kupigia kura vitabadilika kuwa vituo vya
kuhesabia kura baada ya upigaji kura kumalizika.
“Kura zote za urais, ubunge na udiwani zitahesabiwa katika kila kituo na
matokeo yatabandikwa vituoni hapo hivyo sijui wanaosema kura zitaibiwa
zitaibiwaje,” alisema JajiLubuva na kuongeza:
“Baada ya matokeo kubandikwa katika kila kituo yatapelekwa katika kata husika kujumlishwa na hapo pia yatabandikwa.
“Mshindi wa udiwani atatangazwa hapo na yale ya ubunge na urais
yatapelekwa jimboni ambako yatajumlishwa na mshindi wa ubunge
atatangazwa na kukabidhiwa cheti huku ya urais yakipelekwa makao makuu
ya Tume.
“Matokeo ya urais yatabandikwa katika kila jimbo na fomu ile ya matokeo
itaskaniwa na kutumwa moja kwa moja makao makuu ya tume kwa kupitia
mkongo wa mawasiliano wa taifa badala ya simu za mkononi kama ilivyokuwa
awali,” alisema Lubuva.
Alisema njia hiyo itasaidia matokeo kufika kwa haraka kama inavyotakiwa
na baada ya tume kupokea matokeo hayo itakuwa ikiyatangaza moja kwa
moja kupitia luninga na redio.
Jaji Lubuva alisema njia nyingine iliyoandaliwa ya kutuma matokeo ni
kwa nukushi (fax) ambako halmashauri zote nchini zimepatiwa vifaa
vitakavyoziwezesha kuyatuma matokeo haraka.
Alisema hatua ya tume kutangaza matokeo hayo kupitia luninga na redio
itasaidia wananchi kulinganisha matokeo watakayokuwa nayo na
yatakayokuwa yanatangazwa na tume.
Kutokana na hali hiyo alivishauri vyama vya siasa viache kauli za
kuwataka wafuasi wao wasiondoke vituoni baada ya kupiga kura kwa vile
hakuna kura zitakazoibiwa.
“Sioni haja ya vyama kusema vinalinda kura kwa sababu kura zote zinabaki
vituoni na zitahesabiwa palepale tofauti na zamani ambako zilikuwa
zikipelekwa kata na jimboni kuhesabiwa,” alisema.
Jaji Lubuva pia alivitaka vyama vya siasa kuacha kuingilia majukumu ya
Tume hiyo ikiwamo kuhoji mabadiliko ya watendaji yanayofanywa ndani ya
taasisi hiyo.
“Navishauri vyama vya siasa viache kuingilia majukumu ya Tume, haviwezi
kutuchagulia na kutuambia pale weka karani fulani hapa fanya hivi…
waache kuingia jikoni wasubiri chakula kipikwe watakula kwa haki wala
wasiogope,” alisema.
Ametoa kauli hiyo siku chache baada ya vyombo vya habari kumnukuu
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akisema
Mkurugenzi wa Tehama wa Tume hiyo, Sisti Cariah ameondolewa katika
nafasi hiyo huku akihusisha mabadiliko hayo na maandalizi ya kuiba
kura.
Hata hivyo NEC ilikanusha taarifa hizo ikisema hakuna mtu yeyote
aliyehamishwa katika idara zake zote isipokuwa wakuu hao wa idara
walichelewa kuwasilisha picha zao ndiyo sababu hawajaingizwa katika
orodha iliyomo katika tovuti ya Tume.
Jaji Lubuva alisema daftari la mwisho la wapiga kura litakamilika baada
ya wiki mbili hadi tatu na wapiga kura watapata fursa ya kulihakiki kwa
siku nane kabla ya uchaguzi.
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Home » Unlabelled » Ni Marufuku Kusafirisha Masanduku ya Kura......Tume Yasisitiza Matokeo Yatatangazwa Vituoni, Fomu za Urais Kuskaniwa Jimboni na Kutangazwa LIVE
Post a Comment