Wakizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi katika wodi namba tatu na namba nane walikolazwa, majeruhi hao wamesema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM ambao walikuwa katika makundi makundi kati ya saa mbili na saa nne usiku.
Nteminyanda ambaye ni mkazi wa Kisesa Mwanza amesema kuwa aliitwa na mgombea ubunge wa CCM, Michael Kembaki na kufikia katika hoteli ya CMG ambapo kulikuwa na kikao cha chama hicho lakini alianza kuhojiwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho. Lakini licha ya kutoa vitambulisho vya kazi wafuasi hao walianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga mwilini na kuanguka chini. Hata hivyo watu hao waliendelea kumkanyaga hadi akapoteza fahamu.
Wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitalini ambapo alipewa kitanda namba tatu cha wodi namba tatu.
“Waliokuwa wakinishambulia walikuwa vijana wengi kutokana na kunikabiri vibaya sikuwatambua kwa haraka lakini wakiwekwa kwenye mstari wa utambuzi nitawatambua” amesema Nteminyanda.
Wengine waliojeruhiwa ni Waiboga warioba (37) aliyekatwa kichwa na sikio la kulia,Busiro Rhobi (28) mkazi wa Nyamongo aliyekuwa na gari lake binafsi, Daniel Mathew (18) mkazi wa Goribe Wilayani Rorya anayedaiwa kupigwa risasi kichwani upande wa kulia na mgombea udiwani wa kata ya Ikoma Laurence Andriano (CCM).
Wengine ni Wambura Marai (38) aliyeopolewa kutoka kwenye gari lake baada ya kutokea ubishani kati yake na wafuasi wa CHADEMA kuwa mshindi urais atakuwa John Pombe Magufuli.
Rose Hosea muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Tarime amesema kuwa wakati wanapokelewa hali yao ilikuwa mbaya zaidi lakini kutokana na juhudi za timu ya wauguzi wa zamu walitoa huduma za haraka ikiwa ni pamoja na kuwashona majeraha yao huku wakiwapa dawa za maumivu.
“Hali yao inaendelea vizuri kwa sasa tofauti na ilivyokuwa jana” amesema Hosea.BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.



Post a Comment