CHICKENS coming home to Roost
Mara baada ya JFK kupigwa risasi kule
Dallas na kufariki dunia, wana habari walikwenda kwa Malcolm X kumuuliza
maoni yake na jibu lake lilikuwa fupi tu "The Chickens came home to
roost"
Kwa ufupi tu, X alieleza namna serikali
ya Marekani ilivyoachia wazungu kunyanyasa, kuua na kutesa watu wa rangi
nyingine kama Waafrika, bila ya kuwachukulia hatua yoyote. Hivyo, sasa
weupe nao umefika wakati wapate madhila pia. Wamarekani walimlaani X kwa
ajili ya kauli hiyo lakini ulikuwa ukweli.
Hiyo ndiyo hali inayomkuta Dk. Wilbrod Slaa hivi sasa. KUKU wake nao sasa wameanza kurudi bandani.
Kwa miaka takribani saba au nane sasa, Dk. Slaa alikuwa akishuhudia
namna vijana wa chama chake walivyokuwa wakitukana watu mitandaoni,
wakizushia watu mambo yasiyo ya kweli, wakidhalilisha na kuondoa utu wa
watu.
Wakifukuzisha watu kazi kwa tuhuma za uongo, wakiharibu credibility ya
watu walio credible na kumaliza maisha ya kisiasa ya watu ambao siasa
zao zingekuwa na msaada mkubwa kwa taifa huko tuendako. Wote hawa
waliharibiwa na Propaganda Machinery ya CHADEMA.
Nimeona watu wakilia machozi kwa kuumizwa kihisia na vijana wa CHADEMA,
nimeshuhudia watu wakinyimwa kabsa haki ya kujieleza kwa sababu ya
kuzidiwa na nguvu, shinikizo na kashfa za vijana wa chama hicho.
Kama isingekuwa tu uvumilivu wa aina yake, leo hii Zitto Kabwe angekuwa
amekufa kabisa kisiasa au kimwili. Hii kazi ilifanyika vizuri na Dk.
Slaa alikuwa miongoni mwa wafaidika wa siasa za namna hii.
Wakati huo, yeye alikuwa UNTOUCHABLE... Mguse Slaa uone kitakachokukuta.
Sasa leo, wafuasi wa kwenye mitandao na magazeti yaleyale yaliyokuwa
yakimpamba na kumlinda kwa gharama yoyote, yameingia katika kazi ileile
waliyozoea. Kwa bahati mbaya, mara hii Dk. Slaa ndiyo muathirika. Hiki
anachokipata sasa, ndicho ambacho akina Zitto wamekuwa wakiishi nacho
kwa miaka sasa.
Now, the Chickens are Coming Home to Roost, Dr. Slaa.
Post a Comment