BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Wilbroad Slaa.
HOTUBA
ya kwanza tangu ‘atoweke’ kwenye anga za siasa ya aliyekuwa Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Wilbroad Slaa,
aliyoitoa juzi Jumanne juu ya kujiweka pembeni, imepokelewa kwa hisia
tofauti huku wengi wakimuita kuwa ni shujaa wa taifa kutokana na ujasiri
wake, Ijumaa lina kila kitu.
Katika
mahojiano yaliyowahusisha wananchi na wachambuzi mbalimbali wa mambo ya
kisiasa kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mara baada ya kiongozi
huyo kukutana na waandishi wa habari, waliliambia Ijumaa kuwa, Dokta
Slaa ni mtu wa aina yake ambaye taifa halijapata kuwa naye tangu
kuondoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe.Ana msimamo
Wengi
walionesha kufurahishwa na misimamo ya kiongozi huyo tangu ajiingize
kwenye masuala ya siasa, kwani siku zote amekuwa mstari wa mbele
kuwatetea wanyonge, kuanika maovu na kukemea kila analoliona lipo
tofauti na anavyoamini.
“Kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake
mpeni, Dk. Slaa ni kati ya viongozi wenye msimamo asiyekubali
kuyumbishwa. Amekuwa hivyo tangu nilivyomjua na hata hotuba yake
aliyoitoa juzi, inadhihirisha hilo,” alisema Chande Juma wa Kinondoni
jijini Dar.
Alisema kama mtu alifuatilia vizuri mazungumzo yake, ni
wazi kuwa viongozi wenzake walikubali kubadili msimamo ili kumwezesha
Lowassa aingie Chadema, lakini yeye akakataa licha ya kamati ndogo
kuundwa ili imshawishi alegeze msimamo.
Mgombea urais kupitia Chadema(Ukawa) Edward Lowassa.Rushwa ni adui mkubwa kwake
Mchambuzi
mmoja wa habari za siasa aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema siku
zote anamtambua Dk. Slaa kama mtu mwenye kuichukia rushwa, kwani
anaamini hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayosababisha kero za
wananchi kutoisha, licha ya nchi kuwa na rasilimali za kutosha.
“Unampata
wapi sasa hivi aina ya kiongozi ambaye anaweza kukataa rushwa ya
shilingi milioni 500 akitetea masilahi ya wananchi masikini? Viongozi
wetu wa sasa kila mtu anaweka mbele masilahi yake na familia yake, suala
la kuwatetea wanyonge wanalifanya kama maigizo tu,” alisema mchambuzi
huyo, akikumbushia jinsi mbunge huyo wa zamani wa Karatu alivyokataa
kiasi hicho cha fedha ili ashiriki kuzuia ripoti ya Kamati ya Bunge juu
ya sakata la Richmond isisomwe bungeni.
Maneno kama hayo yalisemwa
pia na mkazi mmoja wa Sinza, Nicholaus John akirejea jinsi alivyokataa
rushwa ya uongozi pale alipoahidiwa kazi nje ya nchi, ilimradi tu
akubali kuachia ubunge wake katika Jimbo la Karatu.
Kwake ni taifa kwanza
Kitendo
chake cha kueleza kuwa alitumia sehemu kubwa ya mshahara wake kumpa
mkewe ili afanye ziara ya kuzunguka nchi nzima katika harakati za
kukijenga chama, ni kielelezo kuwa kiongozi huyo anajali ustawi wa taifa
kwa namna anavyoamini kuliko maisha binafsi ya familia yake.
“Slaa
amekuwa akitanguliza masilahi ya taifa kwenye siasa zake, kama mtu
anakubali yeye na familia yake wale mihogo na maharage ili kipato chao
kitumike kwenye mambo ya siasa, unadhani ana uchungu kiasi gani na taifa
hili?” alihoji Mama Saidi wa Mwananyamala jijini Dar.
Kuweka maisha yake rehani
Kitu
kingine kinachofanya wananchi wengi kumuona Dk. Slaa kuwa ni shujaa wao
ni kitendo chake cha kukubali kuweka maisha yake rehani, ilimradi tu
mambo makubwa na muhimu ya nchi yanasemwa hadharani na kila mmoja
ayasikie.
“Ni nani atakuwa tayari kufa kwa kuwataja watu majina
kwenye uovu, tena watu hao ni vigogo wenye fedha na mamlaka ambao
wanaweza kumfanya lolote. Fikiria kitendo chake cha kutaja majina ya
mafisadi papa wakati ule. Huu ni ujasiri wa aina yake,” alisema Liffa
Jason, mwenyeji wa Shinganya aliye Dar kibiashara.Walisema Dk. Slaa
alifanya hivyo akijua yeye binafsi hafaidiki na lolote, lakini aliweza
kuwataja ili kuwafunua wananchi wawajue watu wanaoitafuna nchi yao.
Hana tamaa
Kingine
kilichoelezwa na watu hao ni kwamba kiongozi huyo hana tamaa ya fedha
wala madaraka, kwani alikubali kuacha ubunge, wenye mshahara na
marupurupu mengi na kwenda kufanya kazi ya kukijenga chama, kitu ambacho
alifanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Lakini kikubwa zaidi, wamedai
kwamba Dk. Slaa angeweza kunyamaza kimya na kufanya kazi ya kumnadi
Lowassa, kwani kwa vyovyote mwisho wa siku angepata kuteuliwa katika
nafasi kubwa na nyeti serikalini.
“Kiukweli hana tamaa, naamini
angekaa kimya na ukatibu mkuu wake wa chama, bado maisha yake yangekuwa
mazuri, kaamua kujiweka pembeni bila kujali athari atakayoipata ili tu
asikumbatie mafisadi ndani ya Chadema,” anasema Elika wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Apewe ulinzi
Kwa kuzingatia mambo yote
yanayoendelea katika maisha yake ya kisiasa, wananchi waliozungumza
suala hili walitaka kiongozi huyo ambaye sasa yuko nchini Italia kupewa
ulinzi, kwani kazi yake kubwa kwa nchi inawakera watu wachache wanaoweza
kumdhuru kwa namna yoyote.
“Unajua tangu siku alipoongea na
kuwalipua viongozi wa Ukawa, ni lazima kutakuwa na vitisho, wengine
wamemtukana na kudai kajidhalilisha, lakini ukweli unabaki palepale kuwa
yeye ni shujaa na anastahili ulinzi ili wasitokee wa kumdhuru,” alisema
Modesta George wa Oysterbay jijini Dar na kuongeza:
“Lakini pia kwa
kila mwenye mapenzi na nchi ya Tanzania, anayechukia ufisadi, rushwa na
uonevu ndani ya vyama vya siasa anayeona kuwa alichokifanya Slaa ni
kitendo cha kishujaa, tuungane kumuombea ili Mungu amuepeshe na balaa.”
Aibomoa VIBAYA Ukawa, aacha majeraha
Kitendo
chake cha kutoa maneno makali kwa viongozi wenzake wa Chadema na Ukawa,
kimesababisha majeraha kwa umoja huo, kwani viongozi sasa wamegawanyika
juu ya nani ni mkweli kati ya yanayosemwa kuhusiana na sakata zima la
Dk. Slaa.
“Dk. Slaa ametuacha njia panda, sasa kama yeye alikataa
kumkaribisha fisadi bila kutimiza masharti, lakini wenzake wakafanya ina
maana sisi sasa tushike lipi?” alihoji Bruno Kei wa Tegeta Kibaoni.
Slaa vs Chadema, Lowassa
Siku
moja baada ya Dk. Slaa kutoa hotuba yake hiyo iliyowasisimua mamilioni
ya Watanzania wenye uchungu na nchi yao, baadhi ya viongozi wa chama
chake wameibuka na kumtetea mgombea wao, Edward Lowassa wakisema
kilichotokea katika kumkaribisha kiliridhiwa na pande zote, akiwemo
katibu huyo.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akihojiwa na
BBC, alisema Dk. Slaa ni mwongo, kwani kama kulikuwa na masharti yoyote
ambayo yeye aliweka kwa ujio wa Lowassa, basi yeye alipaswa
kushirikishwa kama mtu wa sheria, kitu ambacho hakikuwahi kufanyika.
Naye
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia akijibu madai ya Dk. Slaa,
alidai kuwa alichokisema Dokta Slaa ni siasa nyepesi zinazoonyesha
kushindwa.
“Tupambane kwa hoja badala ya uchochezi kwa sababu sisi
sote tutapita ila nchi yetu itabaki, maneno yote ya Dk. Slaa yalijaa
uchochezi ila kwa kifupi ni kwamba, sisi katika Ukawa tupo pamoja na
tunamuunga mkono mgombea wetu.BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment