Loading...

HALI SI SHWARI NDANI YA CHADEMA,DOKTA SLAA AANDIKA KUHAMIA CCM ?

BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWBcG4YaOHHDwKbxfYeScLQ_PYjU8FrYaN6oh-gIdymr4H-KzXr34X2HN_76Hu-5atmb2RgMt4Q8twqQKpV8WiPdjpJizPASqh0f9-L3pAaK20kXXq6XDhGDD3TOgtEODyHHZAPRVUPEw/s1600/slaa-cropped.jpg

Hali ya kisiasa nchini inazidi kuwa tete, kufuatia hatua ya Chadema kukiuza Chama hicho kwa Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa kampuni ya Richmond, Edward Lowassa.

Makubaliano ya Chadema kumuuzia Lowassa Chama hicho yamefanywa Jumapili iliyopita kati ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na Lowassa ambapo Lowassa alikubali kutoa shilingi Bilioni kumi taslim ili aweze kutimiza safari yake ya matumaini ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho,  baada ya jina lake kukatwa na CCM, kwasababu ya makandokando ya Ufisadi yanayomkabili.

Hatua ya Mbowe kukiuza Chama hicho kwa Lowassa imemkera mno Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa. Sababu kubwa ya Dk. Slaa kupinga Lowassa kupokelewa Chadema na kuuziwa chama hicho ili aweze kugombea Urais, ni imani kubwa aliyonayo kwamba Lowassa ni Fisadi mkubwa ambaye alistahili kuwa Gerezani au kunyongwa,  badala ya kupewa heshima ya kugombea Urais katika Chama hicho.

"Kama Lowassa huyu huyu amekatwa na CCM kutokana na ufisadi wake, vipi leo aonekane ni msafi ndani ya Chadema?!", amenukuliwa akihoji na kulalamika Dk. Slaa.

Kutokana na kinyongo hicho alichonacho Dk. Slaa dhidi ya Mwenyekiti wake Mbowe kwa kukiuza chama hicho kwa Lowassa, duru za kisiasa nchini zimebainisha kuwa Dk. Slaa mapema wiki ijayo atafanya maamuzi magumu ya kukihama chama hicho Ili kuachana kabisa na siasa au ikibidi kurejea katika chama chake cha zamani cha CCM.

"Kamwe siwezi kukaa meza moja na Fisadi Lowassa ambaye nilimtangaza kwa kinywa changu mwenyewe katika list of shame pale Mwembeyanga. Ni afadhali hata niachane kabisa na Siasa na ikibidi nirudi katika kazi yangu ya Kanisa kuliko kukaa meza moja na Mafisadi", amenukuliwa akiapa kwa uchungu mkubwa Dk. Slaa ambaye anasifika mno kwa ukali wake wa mapambano dhidi ya Mafisadi hapa nchini.

SOURCE: MWANAHALISI FORUM 27.07.2015BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.

1 comments:

uamuzi wake tu, kama atahamia ccm au kurudi kuwachunga kondoo wa bwana sawa tu

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWS TIME | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top