BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Mwandosya asema Lowassa ni maarufu atakayempuuza apuuzwe yeye
Waandishi Wetu, Dar/mikoani
SIKU moja baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza
rasmi kuondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameibua mjadala mzito kila kona ya
nchi.
Lowassa alijiunga na chama hicho kinachounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) jijini Dar es Salaam juzi huku akisema CCM siyo baba
wala mama yake, hivyo alitangaza kukihama.
Vyama vingine vinavyounda umoja huo ni National League Democracy
(NLD) kinachoongozwa na, Dk. Emmanuel Makaidi, Chama cha Wananchi (CUF)
kinachoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba na NCCR-Mageuzi chini ya
uongozi wa James Mbatia.
Baadhi ya watu wamepongeza uamuzi wa Lowassa kujiondoa CCM kwenda
Chadema kwamba ni wa kijasiri na utafungua milango kwa vigogo wa chama
hicho waliokuwa na hofu kuhama, huku wengine wakiuponda wakisema
hautaweza kukiyumbisha chama hicho tawala.
Kilimanjaro wanena
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Bazili Lema alisema kitendo
cha Lowassa kuhamia chama chao amekipokea kwa mikono miwili, kutokana na
kuwa na imani naye na kusema ujio wake utaleta juhudi za kuhakikisha
wanaiondoa CCM madarakani.
Lema alisema ukiachilia juhudi za kuongeza nguvu katika kuiondoa CCM,
lakini pia kwa viongozi waliokaa katika vyama vya upinzani wanajua
ilivyo kazi ngumu kwa mtu kutoka CCM, na kujiunga na chama kingine cha
siasa, kwani inahitaji kujitoa sadaka, kujituma kwani CCM ni chama dola
kinachotumia ubabe katika kuendesha siasa.
Alisema CCM ni ngome ya wezi na mafisadi katika nchi hii, na kudai
kuwa ufisadi haupo kwa mtu mmoja mmoja badala yake upo ndani ya chama.
“Akitokea mmoja anatoka kwenye bahari ya CCM, na kuingia katika vyama
vya upinzani maana yake yuko tayari kusaliti ufisadi wa CCM, hivyo ni
ushindi kwa wanaopigania haki, wanaopigana kupambana na ufisadi
wamembatiza na kumwondolea dhambi ya ufisadi aliyokuwa nayo CCM,”
alisema Lema.
Lema alidai kuwa Lowassa kujiunga na Chadema yuko tayari kuhakikisha
anapigania kuondoa ufisadi ndani ya nchi yetu, na kudai kuwa panya
aliyeamua kuhamia chumba cha paka, na kama hatakuwa na tabia za paka
hawezi kuishi.
Alisema kilichomuondoa Lowassa ni tabia za CCM kuoneana,
kudhulumiana, kunyanyasana, ununuzi wa kura zimemfika shingoni na
kushindwa kuvumilia.
Aliongeza kuwa CCM walikuwa wakiangaika usiku na mchana kuhakikisha
kuwa Lowassa hajiungi na Chadema, lakini sasa amejiunga na Chadema,
hivyo wanachofanya si kupambana na Lowassa na badala yake wanapambana na
Chadema.
Katibu CCM
Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Deogratius Rutt alisema miongoni
mwa watu walioamini na kupewa heshima kubwa ni Lowassa na hakutegemewa
kufanya kitendo kama hicho.
Rutt alisema anawashangaa Ukawa kwa kitendo cha kumpokea Lowassa,
kwani walikuwa mstari wa mbele kuwaambia wananchi kuwa Lowassa fisadi,
mwizi iweje leo wanampokea na kudai Lowassa jembe.
Alisema Chadema walidai kuwa hawawezi kupokea makapi kutoka CCM,
lakini mtu aliyekuwa akigombea nafasi ya urais kupitia CCM na kukosa
sifa wao ndiyo wanamchukua.
Kuhusu kupasuka kwa chama baada ya Lowassa kuhamia Chadema, Rutt
alisema chama hakikubebwa na Lowassa, hivyo kutoka kwake hakuwezi
kusababisha mpasuko na kwamba kila mmoja ana uhuru wake wa kuamua
anakwenda chama gani.
Elizabeth Juma alisema kitendo cha Lowassa kuhamia chama kingine ni
haki yake, lakini pia wananchi wana wajibu wa kuchagua kiongozi
atakayewaletea maendeleo na si kuangalia anapendwa na watu au anatokea
chama gani ili mradi anafaa kuwaongoza.
Jamal Rajabu alisema kitendo cha Lowassa kuhama chama amefurahi na
kusema itakuwa fundisho kwa CCM kutenda haki katika kura zao za maoni na
si kumbeba mtu kwa kuwa wanajua watapata manufaa ndani ya chama hicho,
kwani wananchi hawataki kuchaguliwa Rais.
Mbeya wafunguka
Mwenyekiti wa Chama cha Wazabuni Mkoa wa Mbeya, Yahaya Lema ameunga
hatua ya Lowassa kujiunga upinzani kwa madai kutaimarisha demokrasia ya
kweli hususan kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Alisema uamuzi wa kiongozi huyo wa juu kutoka CCM haupaswi
kuchukuliwa kwa mtazamo hasi, bali kama changamoto ya kidemokrasia na
kwamba utasaidia kuimarisha na kuleta uwiano wa kisiasa nchini.
Mwenyekiti wa APTT-Maendeleo, Godfrey Mwandulusya kwa upande wake
alisema kuondoka kwa kiongozi huyo kumetokana na ufinyu wa demokrasia
ndani ya vyama vya siasa nchini, kwani haki yake iliporwa kwa kuwa
chombo kilichomuengua hakikuwa na mamlaka hayo kwa mujibu wa kanuni za
chama chake cha zamani.
Aliongeza kuwa kutokana na hatua hiyo ya Lowassa kujiunga upinzani
kutashuhudia uchaguzi wenye kinyang’anyiro kikali dhidi ya chama tawala
na vile vya upinzani vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kamishina wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala
alisema,”binafsi napongeza uamuzi mgumu wa Lowassa kujiunga Ukawa
kupitia Chadema, amefungua milango mipana ya demokrasia nchini na
kuwatoa minyororo wale waliokuwa wanadhani siasa za upinzani ni uadui,”
alisema.
Aliongeza kuwa kuhama kwa Lowassa kutaleta tija ya vyama na watawala
wajao kwani kitendo chake hicho kinaashiria kizazi kilichopo kiamue
hatima ya taifa lijalo.
Ezekiel Kipigapasi, mkazi wa Mbalizi jijini Mbeya, alisema Lowassa
kafanya uamuzi sahihi kwa malengo ya kisiasa aliyojiwekea, lakini si
rahisi kutimia kwa kuwa atahitaji kuungwa mkono na wafuasi wake
aliowaacha ndani ya CCM.
“Labda kama ataondoka na sehemu kubwa ya wenyeviti wa CCM wa mikoa na
wilaya, lakini ninavyoona si rahisi, hivyo kwa kuwa CCM na mifumo yake
ya kiutawala haitakubali kuona wanadhalilika kwa kuruhusu kupoteza
katika uchaguzi mkuu,” alisema Kipigapasi.
Kipigapasi alisema hata kama idadi kubwa ya wana-CCM walikuwa
wanamuunga mkono kwenye mchakato wa kura za ndani za maoni ya chama
hicho hawatakuwa tayari kumfuata kiongozi huyo kwa kuwa wengi wao wana
hofu ya kupoteza nafasi zao.
Omar Mruma yeye alisema siasa za sasa ni biashara, kila mtu
anaangalia wapi anaweza kufanikiwa kirahisi, hivyo uamuzi wa kiongozi
huyo unalenga zaidi maslahi yake binafsi na si taifa au wananchi.
Arusha usipime
William Laizer alisema hatua ya Lowassa kuhama CCM ni haki yake ya kikatiba.
Alifafanua kwamba mpasuko wowote utakaotokea ndani ya CCM utakuwa
umesababisha na viongozi wachache wa chama hicho waliosimamia mchako wa
kumpata mgombea urais ndani ya chama hicho.
Elizabeth John alisema alichotendewa Lowassa si cha haki ndani ya CCM
kwa kutambua kuwa CCM ni chama ambacho siku zote kimekuwa ni chama cha
kutumia demokrasia katika utoaji wa uamuzi wake wote.
“Uamuzi uliofanyika Dodoma wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa
nafasi ya urais ndani ya CCM ulifanywa na kikundi cha watu wachache bila
hata kuwahoiji watia nia wote waliojitokeza nguvu ya udikteta ilitumika
zaidi wakati wa mchakato huo,” alisisitiza Elizabeth John.
Anton Mathayo alisema Lowassa ana akili timamu, ana uamuzi wa utu
uzima alichoamua ni haki yake na wala hakulazimishwa na mtu yeyote.
Eliewaha Mmbaga kutoka Kijiji cha Mhezi alisema Tanzania inahitaji
kiongozi ambaye ataisaidia nchi kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo.
Mkazi wa Arumeru, Monica Charles aliema Lowassa angepaswa kuwa
mtulivu licha ya kwamba CCM si baba yake wala mama yake, lakini akumbuke
hicho ndicho chama kilichomlea maisha yake yote akiwa katibu msaidizi.
Kwa upande wake, mkazi wa Kijiji cha Masaera, Celina Minja alisema
Lowassa asingepaswa kuhama chama bali alipaswa kukubali yote
yaliyotokea, kwani hatua ya kwenda upinzani ni kukidhalilisha CCM.
Alisema wapo viongozi wengi waliojitosa nafasi hiyo wa ngazi ya juu katika taifa lakini wamekubaliana na matokeo.
Tabora wamvulia kofia Lowassa
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tabora, Idd Shaaban Kapama alisema kila
mtu ana haki ya kidemokrasia kuamua aende chama gani pasipoingiliwa na
mtu yeyote yule hasa anapoona hajatendewa haki na chama chake.
Alieleza wazi kuwa kama atapitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kugombea urais mwaka huu watakipa wakati mgumu CCM katika
uchaguzi ujao kwani Lowassa anakubalika na watu wengi na ana ushawishi
wa kisiasa.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Tabora, Athuman Balozi
alisema uamuzi wa Lowassa kuachana na chama chake ni wa busara, kwani
CCM si chama pekee hapa nchini na si baba yake wala mama yake kama
alivyodai.
Kada na Mhamasishaji Mkuu wa Chadema Mkoa wa Tabora, Daudi Elisha
alipongeza uamuzi huo na kueleza kuwa sasa Ukawa wamepata jembe la nguvu
na kutoa mwito kwa makada wengine wanaotendewa ndivyo sivyo ndani ya
CCM kujiunga na chama hicho ili kuongeza nguvu zaidi ya kukiondoa
madarakani chama tawala.
“Lowassa hana ubaya wowote na wala si fisadi ndiyo maana
hakushtakiwa, tatizo lililopo ni mfumo mbaya wa utawala ndani ya CCM
ambapo kila anayeingia atachafuliwa tu, hata Magufuli si safi labda
atoke huko,” alisema.
Mratibu wa Chadema Kanda ya Magharibi, Christopher Nyamwanji
alipongeza hatua ya kiongozi huyo kujiunga na chama hicho na kuwataka
wana-Chadema wote kuwa kitu kimoja na kumpa ushirikiano wa hali ya juu
na wenzake watakaohamia Ukawa.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tabora Mjini, Saimon Lameck alisema
wao hawana kinyongo na makada wanaohamia chama hicho kutoka vyama
vingine, wanawakaribisha kwa mikono miwili.
Lowassa
Akizungumzia kujiondoa CCM jijini Dar es Salaam juzi, Lowassa alisema
yaliyotokea Dodoma ameyatafakari na kwa mantiki hiyo atakuwa mnafiki
kuendelea kubaki CCM.
Kuhusu Richmond Lowassa alisema yaliyotokea Dodoma, yamelitia dosari
taifa na kwamba CCM aliyoiona Dodoma si ile ambayo amekulia kisiasa.
“Kama mtu aliye na uchungu na nchi yake nasema basi. Kama Nyerere
(Julius) alivyosema CCM, si baba yake na si mama yake hivyo leo (juzi)
nasema CCM si baba wala mama yangu, kama ni mabadiliko tutayapata nje ya
CCM ambapo kuanzia leo (jana) nipo Chadema,” alisema Lowassa.
Pia, alisema alitangaza kugombea urais kupitia CCM mkoani Arusha
pamoja na yaliyokea Dodoma bado safari yake ya matumaini ipo pale pale
na kwamba alipewa hamasa na umati wa wananchi wakati akitafuta wadhamini
mikoani kote.
Imeandikwa na Joyce Anael, Richard Mwangulube, na Odace RwimoBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment