Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichosafiri na staa huyo ambaye yupo nchini humo kwa ziara yake inayofahamika kama ‘Nana Tour’, tangu Diamond alipofika siku ya kwanza akiwa na mameneja wake, Salam, Babu Tale, DJ wake aitwaye Romy Jones na wengine, mastaa kibao wakubwa walikuwa wakihitaji kuwa wenyeji wake.
- “Jamaa ana uhusiano mzuri sana na mastaa wa Nigeria. Kuna ambao ameshafanya nao kazi kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Bracket, Iyanya, KCEE na P Square (bado haijatoka).
- “Pia wapo wengine kibao wanaotaka kufanya naye kazi hivyo wanamuwinda.Waliposikia anakuja kufanya ziara ya wimbo wake mpya kila mmoja alitaka kuwa mwenyeji wake.
“Simu zilikuwa nyingi lakini mwisho wa siku KCEE alikuwa ameshafika uwanja wa ndege kutupokea na hiyo ilikuwa rahisi kwake kwa kuwa naye hivi karibuni alimshirikisha katika wimbo wake wa Love Boat,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kinaendelea kumwaga ubuyu kuwa baada ya kufika nyumbani kwa KCEE, staa huyo mwenye mikoko na majumba ya kutosha nchini humo kupitia muziki, aliwafanyia bonge la ‘sapraiz’ kwa kufungua makabati yake ya rangi ya dhahabu na kuwaonesha tuzo kibao alizozipata kisha wakajimwaga sebuleni ambapo waliandaliwa pati ya madikodiko ya Kinigeria.
- “KCEE ni kati ya wasanii wenye mafanikio na mali kibao. Jumba tu aliokaribishwa ndani yake lilijengwa kwa kuchanganya nakshinakshi za dhahabu.”
Diamond alitafutwa na mwandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp kuhusiana na mapokezi yake ambapo alifunguka:
- “Nashukuru kwa Nigeria kunipokea vizuri najihisi kama niko nyumbani, nasema asante sana kwa watu hawa kwani wameonesha sapoti ya nguvu hata katika kunipigia kura katika Tuzo za MTV MAMA,” alisema Diamond na kuongeza.
“Kwa sasa akili yangu yote nimeielekeza kimataifa zaidi baada ya kufanya kolabo za kutosha Afrika.”
Hivi karibuni Meneja wa Diamond, Babu Tale alikaririwa akisema kuwa mashabiki wategemee kolabo ya kimataifa na msanii mkubwa na kudokeza kuwa msanii huyo anaweza kuwa Usher Rymond, Chris Brown, Ne-YO au yeyote mkubwa kutoka MarekaniBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Post a Comment