Muda mfupi baada ya kuwapo taarifa kuwa Magufuli anaongoza kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu, aliongezewa ulinzi usiku huo na hadi jana muda wote, alionekana akiwa na walinzi watano.
Chato/Dar. Saa chache baada ya Dk John Magufuli
 kutangazwa kuwa mteule wa CCM kuwania urais, ulinzi umeimarishwa kwa 
mgombea mwenyewe, nyumbani kwake eneo la Ada Estate, Dar es Salaam na 
jimboni Chato mkoani Geita.
Muda mfupi baada ya kuwapo taarifa kuwa Magufuli 
anaongoza kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu, aliongezewa ulinzi usiku huo 
na hadi jana muda wote, alionekana akiwa na walinzi watano.
Jimboni Chato, nyumbani kwake eneo la Rubambambangwe, polisi walionekana wakitanda tangu jana asubuhi tofauti na siku nyingine.
Askari hao wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya
 Chato, Alex Mkama walionekana nyumbani hapo tangu asubuhi hata kabla 
matokeo yaliyompa ushindi Dk Magufuli  hayajatangazwa.
Mwandishi wa habari hizi ambaye alikwenda nyumbani
 kwa Dk Magufuli kuzungumza familia yake, hakuruhusiwa na polisi 
waliokuwa kwenye lango kuu la kuingilia, walidai wamepewa maelekezo ya 
kutoruhusu watu kuingia.
“Naomba usiingie ndani wala kupiga picha eneo 
hili, hayo ndiyo maelekezo ninayokupa na niliyopewa, vinginevyo mtafute 
RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa) akupe ruhusa,” alisema mmoja wa askari hao.
 Akizungumzia hali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo 
alisema polisi walikuwa wanatekeleza jukumu lao kwa umma la kulinda raia
 na mali zao kutokana na wananchi kwa makundi kusherehekea ushindi wa 
mteule huyo.
Konyo alisema ulinzi huo ulilenga kuweka na kuimarisha usalama kwenye makazi ya familia hiyo.
Hata hivyo, Konyo alipotakiwa kuzungumzia kuzuia 
watu kupiga picha kwenye makazi hayo alikata simu na hata alipopigiwa 
tena hakupokea.
Nyumbani kwake, Ada Estate, ulinzi ulianza 
kuimarishwa mara tu baada ya kiongozi huyo kutangazwa kuwa mgombea wa 
urais kupitia CCM.
Mmoja wa walinzi hao ambaye hakutaka kutaja jina 
lake alisema wameongezwa walinzi wengine wanne mara baada ya matokeo ya 
mjini Dodoma kutangazwa.
Magari kadhaa yenye namba za serikali na magari ya polisi yalionekana yakiingia na kutoka nyumbani kwa Magufuli.
Kadhalika kama ilivyokuwa Chato, walinzi hao 
walisema wamepewa amri kutoruhusu watoto au mwanafamilia yeyote kutoka 
nje au kuzungumza na waandishi wa habari.
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.


 
 
 
 
 
 
Post a Comment