Boniphace Ngumije na Chande Abdallah
MASKINI mtoto huyu!
Unapojaliwa kupata mtoto akiwa mzima asilimia 100 unatakiwa kumshukuru
Mungu. Mwajuma Juma (25) mkazi wa Mbagala, Sabasaba Dar es Salaam,
ameingia kwenye mtihani mzito tangu ajifungue mwanaye Yathib Rajab mwaka
mmoja uliopita, akiwa hana sehemu ya kujisaidia haja kubwa.
Baada ya kugundulika kuwa
na tatizo hilo madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili walimfanyia
opasuaji na kumtoboa kwenye tumbo lake upande wa kulia na kuchomoa
sehemu ya utumbo ambayo imekuwa ikitumika kumsaidia mtoto huyo
kujisaidia.
Akizungumza na Ijumaa juzi,
Mwajuma alisema kuwa madaktari walimwambia kuwa Aprili mwaka huu
alitakiwa kurudi hospitalini hapo ili wamfanyie upasuaji wa
kumtengenezea sehemu ya kutolea haja kubwa.
“Madaktari waliniambia
utaratibu wa kuwasaidia bure watoto wenye tatizo hili umesogezwa mbele
mpaka mwaka 2019. Ili sasa afanyiwe upasuaji zinahitajika shilingi
1,350,000 ambazo sina kwani baba wa mtoto huyo alifariki dunia wakati
nina mimba ya miezi sita.
Naomba msaada kwa Watanzania wenzangu ili mwanangu afanyiwe upasuaji, anateseka sana,” alisema mama huyo.
Post a Comment