INASIKITISHA! Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya
Mount Zion iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili, 47,
(pichani) ameuawa na mwili wake kutupwa ndani ya shule yake baada ya
kupotea kwa zaidi ya miezi sita huku mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi akidaiwa kuwa
mmoja kati ya watuhumiwa wamauaji hayo
Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion
iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili enzi wa uhai wake.
Duru za awali za upelelezi wa polisi, zinamtaja Said kuwa alikuwa na
uhusiano wa karibu na marehemu bila kufafanua alihusikaje na mauaji hayo
ya kinyama yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, siku na tarehe
isiyojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shimo la maji taka ndani ya
eneo la shule aliyokuwa akiimiliki.
Aidha, nyuma ya taarifa hiyo ya mauaji, deni la shilingi milioni mia
tisa (900,000,000) ambalo mwanamke huyo alikuwa akimdai mmoja kati ya
watuhumiwa hao ambao majina yao yote bado hayajafahamika likitajwa kuwa
ndiyo chanzo cha Annah kutolewa uhai.
ALIANZA KWA KUTOWEKA
Wakisimulia kwa uchungu namna Annah alivyotoweka nyumbani kwake, ndugu
wa marehemu walisema, awali Desemba 26, mwaka jana kwenye Sikukuu ya
Boxing Day, kuna wageni walifika nyumbani kwake, Boko, Dar, wakazungumza
na baadaye wakaondoka naye na hakurudi tena.
Mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tatu
Ntimizi, Said Ntimizi anayedaiwa kuwa mmoja kati ya watuhumiwa wa mauaji
hayo.
NDUGU WAPATA WASIWASI, WATOA TAARIFA POLISI
Ndugu hao walisema kuwa siku za kwanza hawakupata wasiwasi kwa vile
ilikuwa kawaida ya marehemu kuwa mtu wa safari kutokana na biashara zake
na kuongeza kuwa walianza kupata wasiwasi baada ya siku nne kupita huku
kukiwa hakuna mawasiliano kati yao na marehemu, jambo lililowalazimu
kuripoti Kituo cha Polisi cha Wazo Hill ambao walianza uchunguzi.
WAUMINI WAFUNGA NA KUSALI
Wakati wote huo, waumini wa kanisa alilokuwa akisali marehemu Annah la
Winners Chapel lililopo Ukonga jijini Dar waliamua kufanya maombi ya
kusali na kufunga kwa ajili ya kumuomba Mungu awaoneshe mpendwa wao
alipo.
MAITI YAPATIKANA SHULENI KWAKE MIEZI 6 BAADAYE
Kwa masikitiko makubwa, ndugu hao walisema, Juni 22, mwaka huu, ikiwa ni
miezi sita na siku na chache tangu kupotea kwa ndugu yao, walipata
taarifa iliyowashtua na kuwaumiza, kwamba mwili wa mpendwa wao
umepatikana ukiwa umeharibika vibaya ndani ya shimo la maji machafu
katika shule yake.
Ndugu, jamaaa na marafiki wakiwa katika misa ya mazishi.
HABARI ZA CHINICHINI
Habari za chinichini ambazo si rasmi zilizonyakwa na Gazeti la Uwazi,
zinaeleza kuwa baada ya marehemu huyo kuchukuliwa nyumbani kwake,
inadaiwa watuhumiwa walikwenda naye mpaka kwenye nyumba ya mganga mmoja
maarufu wa kienyeji (jina kapuni) ambako walimuua kisha kuuchukua mwili
wake na kuutupa shimoni.
POLISI WANASA TUKIO
Kama Waswahili wasemavyo, damu nzito kuliko maji ndivyo ilivyokuwa kwa
Annah ambaye damu yake iliendelea kuwasumbua wahusika kiasi cha unyama
wao kuwafikia polisi kupitia njia za kijasusi na hivyo kufanikiwa
kumnasa mmoja wa watuhumiwa.
“Polisi walipopata taarifa za mauaji hayo, waliamua kufuatilia,
wakabaini mmoja kati ya watuhumiwa hao yuko Arusha. Wakamuwekea mtego na
kufanikiwa kumnasa, wakamleta jijini Dar ambapo aliwataja aliodai
kushirikiana nao,” chanzo kutoka vyombo vya usalama kililiambia Uwazi.
MWALIMU MKUU AZUNGUMZA
Akizungumza na Uwazi, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Dony Maige alisema
shule yake ilikuwa imefungwa wakati marehemu ambaye ni mmiliki na
mkurugenzi akiwa hajulikani alipo.
“Januari mwaka huu, tarehe za mwanzoni tulifungua shule kama kawaida
baada ya likizo ya Desemba ambapo wanafunzi waliendelea na masomo.
Lakini bajeti ilikuwa ngumu kutokana na mkurugenzi ambaye ndiye mtoaji
wa fedha za matumizi ya shule na malipo ya wafanyakazi, kutoonekana.
“Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wazazi kulazimika kuchangia huduma
nyingine muhimu japokuwa walikuwa wamemaliza ada za watoto wao.
MWALIMU AWATOA MACHOZI WAOMBOLEZAJI
“Juni 21, mwaka huu tukiwa tumefunga shule na kutarajia kufungua tena
kwa ajili ya muhula mpya wa masomo, ndipo nilipopokea simu kutoka vyombo
vya usalama na kunitaka kusitisha zoezi la kufungua shule kwa kuwa
kutakuwa na oparesheni maalumu katika eneo la shule. Nikaambiwa
niwaondoe wafanyakazi wote isipokuwa mimi peke yangu.
“Nilishangaa, baada ya kufika shuleni na kuwaona polisi wakiwa eneo la
tukio. Nilishtuka kutokana na maswali waliyokuwa wakiniuliza. Lakini
jambo lililonishtua zaidi ni kuuona mwili wa marehemu Annah ukitolewa
ndani ya shimo la maji machafu lililopo ndani ya shule ambayo kwa miezi
yote sita wanafunzi na hata sisi walimu tulikuwa tukipita bila kujua.
“Kwa kweli sijawahi kukutana na kipindi kigumu kama hiki katika maisha
yangu. Ni jambo la ajabu sana. Nimejiuliza maswali mengi na kukosa
majibu,” alisema mwalimu huyo huku waombolezaji wakishindwa kuzuia
machozi yaliyokuwa yakiwatiririka.
MWILI WAAGWA BILA KUFUNULIWA
Wakati wa kuuaga mwili huo, Jumamosi iliyopita nyumbani kwa marehemu,
waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa masikitiko mbele ya
jeneza la marehemu bila kufunuliwa kutokana na mabaki ya mwili huo
kuharibika vibaya.
Mwili wa marehemu Annah ulipumzishwa katika Makaburi ya Kwakondo, Ununio
jijini Dar. Hakika bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.
Amina. Marehemu ameacha watoto watatu, Steven, Irene na Emerly Mwambili.
POLISI KINONDONI WALIVYOSEMA
Uwazi lilimpigia simu Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Emanuel Mlei na kumuuliza yafuatayo.
Uwazi: “Kuna madai kwamba, mtoto wa aliyewahi kuwa waziri kwenye
serikali ya awamu ya tatu, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi mnamshikilia kwa
mauaji ya mwanamke aliyekuwa mmiliki wa shule, Annah Mwambili, ni
kweli?”
Kamanda: “Kuhusu hilo siwezi kulisema kwa sasa. Ila kesho (jana) nenda
pale kwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova
ataliongelea yeye.”
Uwazi bado liko kazini kuchimba tukio hili la kinyama na kwamba litaendelea kuwaletea mapya kadiri yanavyopatikana
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.


Post a Comment