Loading...

Afariki na mipango ya mazishi ikaanza, ila baada ya siku ya nne akafufuka!

BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
post-feature-image
Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Benjamin Noah Msuya (74), ameanika kwamba, alifariki dunia na mipango ya mazishi ikafanywa lakini siku nne baadaye alifufuka, hapa anasimulia alichokiona baada ya kifo.

Akizungumza na gazeti hili Machi 16, mwaka huu, nyumbani kwake, Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, Msuya ambaye mwaka 1979 aliongoza majeshi ya Tanzania kuingia Uganda kwa mara ya kwanza, alisema kifo chake hicho kilitokana na ugonjwa wa saratani (kansa).

“Awali ya yote, mimi kwa sasa ni Meja Jenerali Mstaafu. Lakini katika utumishi wangu, ndiye niliyeingiza majeshi nchini Uganda mwaka 1979 na kumwangusha mtawala wa mabavu, Idi Amini Dada (sasa marehemu).”
“Baada ya Amini kukimbia, nilikuwa mtawala kwa siku tatu nikimsubiri aliyetakiwa kuwa rais wa mpito, Yusuf Kironde Lule. Lakini sikuondoka Uganda, nikaja kusimamia kuingia madarakani kwa Rais Godfrey Lukongwa Binaisa. Lule alitawala kwa siku 68 tu.”
Akizungumza huku mkewe, Deborah Msuya akimwangalia kwa umakini, meja jenerali huyo alisema alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo akiwa jijini Dar, Desemba, 2010 kwa kutoka uvimbe shingoni upande wa kulia. Alihangaika kwenye hospitali mbalimbali, ikiwemo ya taifa, Muhimbili bila mafanikio wala kuutambua ugonjwa.
“Baada ya kubaini hali yangu inazidi kuwa mbaya na hospitali nchini zimeshindwa kubaini tatizo, nilikwenda Makao Makuu ya Jeshi (Upanga) kuonana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange kutaka msaada wa kwenda kutibiwa nchini Uingereza.
“Sikumkuta, nikakaa ofisini kwake kumsubiri hadi alipofika, nikamwelezea. Mwamunyange alionesha kutoarifiwa kuhusu kuumwa kwangu. Lakini alianza hapohapo kutoa msaada kwa kumwita aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi, Luteni Jenerali Abraham Shimbo (sasa ni balozi nchini China) na kuweka kikao cha kujadili safari ya mimi kwenda kutibiwa Uingereza.”
“Julai 3, mwaka huo mimi na mke wangu, tulisafiri kwenda Uingereza ambako tulipokelewa pia na mwambata wa jeshi, Brigedia Jenerali Pelegreen Mrope. Yeye aliniandalia siku iliyofuata kuonana na daktari wa London Clinic aitwaye Dk. Sheaves.
“Siku niliyokwenda, nilichukuliwa vipimo mbalimbali kama X-Ray, Ultra Sound na MRI (Magnetic Resonance Imaging). Lengo lilikuwa ni kubaini tatizo linalonisumbua. Wenzetu kule wako mbali sana kwa utaalam wa afya.”
Ilikuwa Julai 25, mwaka huo ambapo majibu ya vipimo yalitoka. Hapo ni baada ya kuangaliwa kwa ustadi na Dk. Sheaves na daktari wa kliniki nyingine, anaitwa Dk. Peters wa Hospitali ya London Bridge.
“Vipimo vilionesha nina kansa. Hivyo nikakabidhiwa kwa mtaalam mmoja kwa ajili ya matibabu. Lakini pia nikawa natumia dawa mbalimbali.
“Kuna siku, mtoto wangu anaishi kule anaitwa Bisala au Bis alikuja kunichukua hotelini nikaenda kwake kwenye Mji wa Birmingham ambako siku chache baadaye hali haikuwa nzuri, nikapelekwa kwenye Hospitali ya Heartland ambako Agosti 6, nilifariki dunia. Madaktari walithibitisha na kutoa hati ya kifo.”
“Tayari mke wangu, wanangu wote na ndugu wengine walishapewa taarifa kwamba mimi nimefariki dunia. Hapa nyumbani, Tanzania, kuna jirani yangu aliposikia alikuja mbio hapa nyumbani huku analia.”
“Ndipo kwa siku nne nikapitia kwenye mazito. Mimi kwamba nilikufa sijui, bali nilijikuta nimeingia kwenye maeneo mawili. Niliingia mbinguni na pia niliingia kuzimu. Huko kuzimu kila nikikumbuka naogopa sana. Nilikuta watu maelfu kwa maelfu wakiwa kwenye ziwa la moto. Walikuwa wakilia kwa kuomboleza.
“Midomo na macho yao vilitoa moto. Kila sehemu ya mwili ilitoka moto. Nilipata bahati ya kumsikia Mungu akinena nami juu ya yale niliyokuwa nayaona kuzimu na mbinguni na kuniambia niwatangazie wanadamu wote.
“Mungu aliniambia niwaambie wanadamu kwamba hakuna hukumu. Wengi wanadhani kuna hukumu lakini ukweli ni kwamba hakuna hukumu bali kuna…
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWS TIME | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top