BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Ni Sospeter
Muhongo. Ni takribani mwaka mmoja uliopita, katika kipindi kama hiki,
Profesa Muhongo, akiwa Waziri wa Nishati Na Madini, alijikuta kwenye
mapambano makubwa na makali yenye kuhusiana na maslahi ya kiuchumi.
Profesa
Muhongo alisimama upande wa watu na taifa. Hakuwa na media ya kumsaidia.
Hata hivyo, Muhongo alipambana kijasiri hadi risasi ya mwisho. Ikafika
mahali, na kwa maslahi ya taifa, alilazimika kuingia handakini.
Kwenye Baraza
Jipya lililotangazwa leo, bila shaka, Sospeter Muhongo ni mmoja wa
wateule wenye furaha kubwa ya ' ushindi' . Kwamba ameonyesha kuwa ni mtu
asiyekata tamaa. Aliamua kujimbia handakini. Kimyalimya akapigana
jimboni kwake kuomba kura za wananchi, maana, alikuwa mbunge wa
kuteuliwa tu.
Binafsi
nimefurahi kumwona Sospeter amerudi tena. Niseme wazi, nilimkubali
Sospeter Muhongo kwa utendaji wake na misimamo yake isiyoyumba.
Alisimamia alichoamini ni ukweli na ni kwa maslahi ya umma.
Naaomba hapa nikumbushie nilichoandika Desemba 17, 2014 kwenye ukurasa wangu wa FB;
"Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ameshajiuzuru. Ni hekima na
busara kwa Jaji Werema kuchukua uamuzi huo. Maana, alikiri hata ndani ya
Bunge, kuwa ni kweli kuwa alitoa ushauri wa kuidhinisha fedha kutolewa.
Hata kama ni kwa kuchelewa, bado ni uungwana, kwa Jaji Werema
kuwajibika kwa ushauri aliutoa na hata kuleta mtafaruku wa kisiasa na
kijamii katika nchi.
Hata hivyo,
kuna hamu, miongoni mwa wanajamii, kuwa na kichwa cha Waziri wa Nishati
na Madini, Sospeter Muhongo, nacho kibiringike kwenye vumbi. Hamu hii
inaonekana kupandikizwa pia kwenye jamii ili kutimiza malengo ya
wachache wenye kutaka Muhongo ang'oke kwa sababu zao, ama za kisiasa au
kiuchumi.
Maana, mtu
mzima ukiisoma ripoti ya CAG na kisha PAC, na kisha ukiliangalia jambo
hili kwa macho maangavu, na kwa kuyatafakari mazingira , fursa na
changamoto tulizonazo, kama taifa, kwenye sekta ya madini na nishati, na
kwa kuangalia mwenendo wa harakati za mataifa makubwa kwenye kupigania
rasilimali muhimu kama gesi na mafuta, huoni mantiki ya Tanzania yetu,
pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyonayo Profesa Muhongo, kufanya
maamuzi ya kujitia hasara kama taifa, kwa kumtoa kafara mmoja wa
Watanzania wachache wenye weledi wa kupigiwa mfano kimataifa kwenye
sekta ya madini kwa kuegemea mapendekezo ya ripoti ya PAC iliyoandaliwa
na wanadamu wenye utashi wenye kutofautiana na iliyothibitika, kuwa nayo
ina mapungufu. Na tuwe na ujasiri, kwa maslahi ya taifa, kuyapa mgongo
hata yale ambayo, kwa matashi yetu ya kisiasa hata kijamii, tungependa
yawe ili tunufaike au tufurahi tu, basi.
Ningelikuwa
miongoni mwa wenye kutaka Profesa Muhongo ang'oke, kama ripoti ya CAG
ingeonyesha uhusika wa moja kwa moja wa Profesa Muhongo kwenye sakata la
Escrow. Lakini, ripoti ya CAG haionyeshi hivyo. Na katika kufanya
maamuzi, lililo muhimu ni kutompendelea mtu au kumuonea. Hivyo, ndio
maana ya kutenda HAKI.
Niliouelezea hapo juu, ni mtazamo wangu unaotokana na kusumwa na mapenzi kwa nchi yangu niliyozaliwa, basi."
Maggid Mjengwa,
Iringa.
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment