BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
BIASHARA
imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss
Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond apate
mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah’ miezi
miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani, Risasi Jumamosi
lina ‘full’ stori.Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao,
kimesema makubaliano ya awali baina ya wazazi hao, yalikuwa ni kwa
mwanamke huyo raia wa Uganda, kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa
akisaka ubaba kwa udi na uvumba.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Wote
mnajua jinsi Diamond alivyokuwa akihangaika kupata mtoto, maana wapenzi
wake wote wa awali hawakuweza kumzalia. Sasa alipokutana na Zari ambaye
tayari alikuwa na watoto, wakakubaliana kwa masharti kuwa ndani ya muda
f’lani, amzalie.
Rose akipewa zawadi ya keki na Harmonizer kwa niaba ya Wasafi Classic Baby.
“Sasa
ndiyo ikawa hivyo, baada ya Tiffah kuzaliwa, kila mtu sasa yupo huru
kufanya yake, ndiyo maana Zari amerudi kwake Afrika Kusini ‘Sauz’ na
hawezi kuja kuendelea kuishi na Diamond kama wakati ule wa ujauzito.
“Kule
Sauz, Zari anaendelea na biashara zake na nimesikia kwa sasa anaandaa
Zari All White Party kama ile aliyoifanya Mlimani City hapa Bongo,”
kilisema chanzo chetu.
Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WBC’ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.
KWA NINI HAWEZI KURUDI?
Chanzo
hicho kiliendelea kutoboa siri kwamba, pamoja na makubaliano ya kuzaa,
lakini pia mazingira ya sasa ya makazi ya Diamond hayatoi nafasi kwa
mwanamke huyo mwenye fedha ambaye pia ni msanii, kuweza kuishi.
“Sasa
hivi pale nyumbani kwa Diamond kumejaa, imekuwa familia kubwa. Maana
kuna mjomba wake Diamond anaishi pale, dada zake wawili, Esma na Queen
Darleen wanaishi pale. Mama yake Diamond (Sanura Kasim) yupo pale.
“Haya,
achana na ndugu wengine. Lakini pia kuna wasichana wa kazi wawili na
mlinzi mmoja. Sasa kwa mtu kama Zari ambaye maisha yake ni ya kisupastaa
hawezi kuishi kwenye nyumba yenye watu wengi hivyo.”
ZARI ANAOGOPA UMBEYA
“Pia
inasemekana Zari hataki kuishi na wifi zake kwa sababu anaogopa umbeya.
Hata wakati ule alipokuwa mjamzito mpaka kujifungua, hakuwa mtu wa
kujichanganya nao sana. Alikuwa mtu wa peke yake peke yake tu.”
HAKUNA TENA MAPENZI?
“Taarifa
nilizonazo ni kuwa, Diamond na Zari watakuwa wanaendelea na uhusiano
wao wa kimapenzi lakini si ule wa kama awali. Ila wataendelea kuwa watu
waliozaa mtoto na maisha ya Tiffah yataendelea kuwa kwa mama yake hadi
hapo watakapoamua vinginevyo. Zari anaweza kuja Bongo na Diamond anaweza
kwenda Sauz kwa Zari.”
“Zari hataki kuishi Tanzania, anataka Tiffah
aishi na ndugu zake kule Sauz hadi akue na kuanza masomo. Kwa hiyo
usitegemee ule ukaribu kama wa mwanzo.”
KUHUSU DIAMOND!
Jitihada
za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba
ikielezwa kuwa yupo nchini Marekani katika shughuli za kimuziki. Hata
alipotumiwa meseji kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
Hata hivyo, mtu wake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alitatizwa na suala hili akisema:
“Dah!
Wabongo bwana! Ninachojua mimi ni kuwa, bado watakuwa wapenzi japokuwa
siwasemei maana Diamond naye haaminiki sana. Si unajua ameshapata mtoto,
lolote linaweza kutokea.
“Ila Diamond akimhitaji Zari aje Tanzania
anaweza kuja, akitaka aende Sauz atakwenda kwa sababu Tiffah lazima
alelewe na wazazi wote.
“Halafu lazima ujue kwamba, Zari ni
mfanyabiashara, ana biashara zake Afrika Kusini na Uganda. Kwa hiyo siyo
mtu ambaye unaweza kumtegemea akae sehemu moja tuBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment