BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na
anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa
ameionya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jeshi la Polisi kuchochea
vurugu.
Onyo la Lowassa limekuja ikiwa imebaki siku moja kabla ya Watanzania kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa rais, ubunge na madiwani.
Akihutubia wakazi wa Ifakara Jimbo la Kilombero, Morogoro leo mchana
katika Uwanja wa Shule ya Jagwani, Lowassa amesema “polisi waache
kuwafuatafuata vijana wetu na kuwapiga.”
Lowassa amesema, “Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanapaswa kutambua
kwamba, uchaguzi huu ni muhimu. Watu wamejitolea kujiandikisha na kwenda
kupiga kura ifika Jumapili, watu hawa wana matumaini. Tume itende haki.”
Mbali na onyo hilo, Lowassa amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa
Tanzania, ataanza kutatua changamoto za sekta ya elimu kwa kutoa elimu
bure kwanzia Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu.
“Mbali na elimu, kipaumbele changu cha pili ni kilimo. Nitahakikisha
tunakuwa na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji. Mkulima atakuwa na haki
zake. Serikali yangu itafuta ushuru wa mazao yote. Wakulima watauza
mazao popote watakapotaka duniani,” amesema Lowassa.
Kuhusu maslahi ya wafanyabiashara ndogondogo na wenyeviti wa vijiji
amesema “mimi ni rafiki wa bodaboda, mama lishe na machinga. Nikiingia
madarakani nitaanzisha benki maalum kwa ajili ya makundi haya. Pia
nitawalipa mishahara wenyeviti wa vijiji,” amesema Lowassa.
Lowassa ameahidi kutatua kero za Jimbo la Kilombero ambalo linawakilishwa na mgombea Peter Lijualikali kwa tiketi ya Chadema.
“Kero zinazowakabili wananchi katika jimbo hili ni kutozwa ushuru kwa
wakulima wa mpunga, tatizo la maji, watu wa Sanje kudhulumiwa ardhi
yao, kutokamilika kwa daraja linalounganisha Mahenge, Kilombero na
Malindi na kivuko kilichopo muda wowote kinaweza kuzama,” amesema Lijualikali.
Aidha, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amewataka wananchi kuwahi
katika vituo vya kupigia kura huku kila mpiga kura kubeba kalamu yake
badala ya kutegemea kalamu za maofisa wa NEC.
“Tuwahi katika vituo vya kupiga kura alfajir. Kazi ya kwanza Jumapili
ni kupiga kura, kila mtu aende na kalamu yake. Mtu ambaye hajui kusoma
na kuandika amchukue mwenzake anayemwamini,” amesema Sumaye.
Mbali na wito huo, Sumaye amewataka mawakala wa watakaolinda kura za
vyama vinavyounda Ukawa kutohadaika na rushwa itakayotolewa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
“Kuna dalili kwamba CCM wanataka kuwanunua mawakala wetu. Kweli
unakubali kupewa Sh. 20,000, 30,000 au 50,000 halafu mtoto wako
atesekeke miaka mitano kwa kukosa dawa? Wakala wetu siku hiyo
unapokwenda kwenye kituo chako cha kazi, uwe umekula nyumbani. Usiende
kudoea chai inayoletwa humo, huwezi kufa kwa njaa kwa siku moja,” amesema Sumaye.BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Home » Unlabelled » Lowassa Atoa Onyo kwa NEC na Polisi leo Hii......Sumaye Asema CCM Wamejipanga Kuwanunua Mawakala wa Chadema



Post a Comment