Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko’
kwa mikono huku kikiwatakia kila la kheri baadhi ya makada wake
waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama
na wanaotaka kukihama.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na mtandao huu
jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa
sababu hiyo ndiyo demokrasia.
Aidha, Nape alisema vyombo vya habari vilimnukuu aliyekuwa mgombea urais
kupitia CCM, Edward Lowassa akisema kuwa watu hawawezi kuzuia
‘mafuriko’ kwa mikono na kwamba CCM imeweza kufanya hivyo, lakini habari
hizo haziandikwi.
Alisema wanachama wanaotaka kuhama hawawezi kuzuiwa kwa namna yoyote na
kwamba hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa kada yoyote.
Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais, ulivyokuwa ndani ya CCM,
alisema ulifuata utaratibu na kanuni zote na kwamba kama maneno mengi
yataendelea kusemwa atatoa video inayoonyesha kila kitu kilivyokuwa
ndani ya kikao cha Kamati Kuu (CC).
Kuhusu makada waliokihama chama hicho na kujiunga na Chadema, Nnauye
alisema baada ya Baraza la Madiwani kuvunjwa hapakuwa tena na
wawakilishi wa aina hiyo.
Post a Comment