RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amevunja ukimya kuhusu namna mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, ulivyokuwa mkoani Dodoma mpaka akapatikana Dk John Magufuli.
Mwinyi
ambaye ni sehemu ya Baraza la Wazee la CCM, lenye mamlaka na ushawishi
katika vikao vyote vya juu vya chama hicho, alizungumzia mchakato huo
jana alipokuwa akitoa salamu za Sikukuu ya Idd, baada ya kumaliza swala
katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
“Mambo
yalikuwa magumu kidogo kule Dodoma, lakini tunashukuru Mwenyezi Mungu
jahazi lilifika salama, kwa pamoja tuendelee kuwa watulivu hadi Uchaguzi
Mkuu utakapofika na tuilinde amani,” alisema Mzee Mwinyi.
Mzee
Mwinyi alimshukuru Mungu akisema japo mambo yalikuwa magumu wakati wa
mchakato wa kumtafuta mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, suala hilo
lilimalizika salama bila kuwepo kwa tatizo lolote.
Alisema
Uchaguzi Mkuu utakapofika mwezi Oktoba, Watanzania wanapaswa kuchagua
viongozi wazuri watakaoleta amani, mapatano na maendeleo.
Alitaka
Watanzania waachane na fikra za kibaguzi kwani hakuna aliye bora kuliko
binadamu mwingine hapa duniani, huku akishauri waumini wa dini zote
kuombea Taifa lipite salama katika uchaguzi huo.
Ugumu wenyewe
Ingawa
Mzee Mwinyi hakutaka kufafanua kuhusu ugumu huo, lakini moja ya mambo
yaliyoashiria ugumu wa mchakato huo, ilikuwa kujitokeza kwa wawania
urais 42 kupitia chama hicho waliochukua fomu, huku 38 kati yao
wakirejesha na kutoa nafasi kwa vikao vya chama hicho, kukabiliana na
ugumu wa kuchambua majina yanayotakiwa kufanyiwa uamuzi na vikao mbali
mbali vya chama.
Rais
Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM naye alikiri ugumu huo
alipokuwa akitoa hotuba ya kuaga wabunge, ambapo alisema wagombea
wamejitokeza kwa wingi na wengi ni vigogo na kuwashauri wasinune baada
ya vikao vya chama kufanya uamuzi.
Miongoni
mwa vigogo hao ni pamoja na wasaidizi na washauri wakuu wa Rais
Kikwete, ambaye alishaweka wazi msimamo wake kuwa hana mgombea, akiwemo
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
V
i g o g o w e n g i n e ni pamoja na mawaziri wakuu w a s t a a f u , a
k i w e m o F r e d e r i c k Sumaye wa Awamu ya Tatu na Edward
Lowassa, aliyeongoza katika miaka miwili ya mwanzo ya Serikali ya Awamu
ya Nne.
Pia
kulikuwa na mawaziri wengi wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete,
wakuu wa zamani wa Taasisi ya Usalama wa Taifa, mabalozi, wabunge na
makada wengine wa CCM, wenye sifa za kitaifa na kimataifa, mvuto na
nguvu ya ushawishi katika nafasi hiyo.
*Mchujo wa vikao
Ugumu
mwingine ulioonekana, ulikuwa kazi ya mchujo ambayo kwa kuongozwa na
vigezo vilivyokuwa bayana, ilianza na vikao vya mashauriano, ikafuatiwa
na kikao cha Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili na kuingia katika Kamati
Kuu ya CCM, ambayo ilitakiwa kupitisha panga kali na kuja na wagombea
watano.
Kamati
Kuu iliyoongozwa na Rais Kikwete ilifanya kazi yake na kuja na majina
ya makada watano, kati ya hao mawaziri ni wanne akiwemo wa Ujenzi, Dk
John Magufuli, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Balozi wa Umoja wa Afrika
nchini Marekani, Amina Salum Ali.
Ugumu
wa upatikanaji wa majina hayo yaliyopelekwa kikao cha Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) ya CCM, ulijidhihirisha kwa kuwa hata washauri wa karibu
wa Rais Kikwete; yaani Makamu wa Rais Dk Bilal na Waziri Mkuu wake
Pinda, pamoja na mawaziri wakuu wa zamani, Sumaye na Lowassa, hawakuwamo
katika majina matano ya awali.
Tukio
la baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, Dk Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba
na Adam Kimbisa kujitenga na uamuzi wa kikao walichoshiriki, ni moja ya
kielelezo cha ugumu huo.
Hata
hivyo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alifafanua kuwa
uamuzi wowote katika vikao unafanyika kwa kura, ambapo wengi hupewa na
wachache husikilizwa, akimaanisha kuwa wajumbe wengi wa Kamati Kuu zaidi
ya 30 waliridhia majina hayo matano, isipokuwa hao watatu.
Ugumu NEC
Wakati
wa ufunguzi wa vikao vya NEC uliokuwa wazi, baadhi ya wajumbe waliimba
nyimbo za kumsifu Lowassa, ambaye ni mmoja wa wagombea vigogo, ambaye
jina lake halikuwa miongoni mwa majina matano yaliyopaswa kujadiliwa na
kupigiwa kura na NEC.
Hata
hivyo, taarifa za ndani zilieleza kuwa wajumbe hao wa NEC baada ya
kujadiliana, waliridhia kwa umoja kupigia kura majina hayo matano
yaliyopendekezwa na Kamati Kuu, ambapo Dk Magufuli, Balozi Amina na Dk
Migiro walipita na majina yao kwenda katika kikao cha Mkutano Mkuu.
Usalama wa jahazi
Huenda
kauli ya Mzee Mwinyi kuwa jahazi lilifika salama, ilimaanisha katika
Mkutano Mkuu uliooneshwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali, kwani
tofauti na ilivyokuwa katika vikao vingine hasa Kamati Kuu na NEC,
Mkutano Mkuu ulidhihirisha uimara na umoja wa chama hicho, ambapo
wagombea walipata nafasi ya kujieleza na kupigiwa kura na wajumbe.
Uchaguzi
huo wa kumpata mgombea wa CCM, uliweka historia ambapo kwa mara ya
kwanza katika historia ya chama hicho, tangu wakati wa kupigania Uhuru,
wakati huo ikiwa Tanu na baadae Tanu ilipoungana na ASP kuunda CCM,
wanawake wawili walipenya kuingia katika Mkutano Mkuu.
Kukubalika
kwa uamuzi wa Kamati Kuu na NEC, kulijidhihirisha katika Mkutano Mkuu
uliofanyika kwa shangwe, ambapo baada ya kura, Dk Magufuli aliibuka na
ushindi wa kishindo wa baada ya kupata kura 2,104 kati ya kura halali
2,416, sawa na asilimia 87.1 ya kura zote.
Balozi
Amina alifuata kwa kupata kura 253 sawa na asilimia 10.5 huku Dk Migiro
akipata kura 59 sawa na asilimia 2.4, huku kura sita tu zikiharibika,
jambo lililodhihirisha kuwa CCM ni moja, imempata mgombea wake kwa umoja
na kufifisha mgawanyiko na hofu iliyotokana na vikao vya awali, hasa
Kamati Kuu na NEC.
Post a Comment