BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
CHARLES
Makongoro Nyerere (CMN) ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliotangaza
nia ya kutaka kuchaguliwa kuwania urais kupitia chama hicho mwaka huu.
Raia Mwema lilifanya naye mahojiano wiki hii nyumbani kwake jijini Dar
es Salaam. Endelea
-RAIA MWEMA: Kwanini wana CCM wanatakiwa wakuchague wewe uwe
mgombea wao na si mwingine miongoni mwa wenzako 41 waliojitokeza kuwania
nafasi hiyo?
MAKONGORO: Mimi si mwizi, wala mla rushwa. Nina uzoefu wa kutosha na
nakijua chama changu. Pia ni mtu ambaye napenda kufuata utaratibu. CCM
sasa inahitaji mtu wa namna hiyo.
-RAIA MWEMA: Kwanini unadhani uadilifu ndiyo sifa kuu ya Rais ajaye wa Tanzania?
MAKONGORO: Naamini kuwa ni mtu mwadilifu pekee ndiye ambaye
ataisaidia nchi yetu kuondokana na matatizo tuliyonayo. Ufisadi, wizi wa
mali ya umma na matatizo yote tuliyonayo yataondoka endapo tutampata
kiongozi ambaye ni muadilifu.
Kinachotakiwa ni kwa chama kujisafisha chenyewe kwanza. CCM ikiwa safi,
serikali itakuwa safi tu. Lakini serikali haiwezi kuacha kuwa ya
kifisadi wakati chama chetu kina mafisadi na tunawavumilia.
-RAIA MWEMA: Ina maana kama utafanikiwa kuwa Rais na hatimaye Mwenyekiti
wa CCM unaweza kuwafukuza wanachama wote wenye tuhuma za ufisadi?
MAKONGORO: Hapana, siwezi kumfukuza mwanachama kutoka CCM.
Tunachoweza kufanya ni kuwatoa kutoka katika nafasi zao za uongozi.
Nitakupa mifano miwili kueleza hili.
Kwa mfano wewe ni Mwislamu. Dini yako inataka uwe unaswali swala tano
kwa siku. Sasa pale msikitini kwako una Imamu ambaye kwa siku
anahudhuria swala moja au asihudhurie kabisa. Lakini kila siku unaambiwa
anaonekana klabu ya pombe akinywa.
Sasa huyu imamu dawa yake si kumvua Uislamu wake. Unachofanya ni kumtoa kwenye uimamu na kumpa mtu mwingine ambaye hatawakwaza.
Kama wewe ni Mkristo na una Paroko ambaye kila kukicha ana kashfa za
ngono na wake za watu ingawa hajawahi kukutwa huyo si paroko. Sasa
ikitokea siku akanusurika kufumaniwa hadi akaacha mavazi yake ya uparoko
kule Guest House lakini akachoropoka bila kukamatwa; huyo humvui
Ukristo wake. Unachofanya ni kumtoa kwenye Uparoko wake.
Chama ni imani kama zilivyo dini. Huwezi kumwondoa mtu kwenye chama
lakini unaweza kumwondoa kwenye nafasi za uongozi. Kwa kifupi, kuna
maparoko na maimamu wa aina hiyo ndani ya CCM ambao ni lazima kuwaondoa
kwenye nafasi zao kama kweli tunaitakia mema nchi yetu.
-RAIA MWEMA: Unasema chama ni imani lakini wewe uliondoka CCM na kuhamia
NCCR Mageuzi kwenye miaka ya 1990. Ilikuaje ukahama chama chako?
MAKONGORO: Mojawapo ya matatizo ya chama chetu ambayo ni lazima Rais
ajaye apambane nayo ni ukweli kwamba kuna majimbo ya uchaguzi hapa
Tanzania ambayo kama mtu hutoi rushwa huwezi kupita.
Arusha ni mojawapo ya maeneo hayo. Yaani kama hula hela sahau kuhusu
kuchaguliwa. Utafanyiwa mizengwe na viongozi wala rushwa hadi mwenyewe
utachoka na kukata tamaa.
Mimi mwaka ule wa 1995 nilikumbwa na tatizo hilo. Nilitaka ubunge pale
Arusha lakini mtandao wa rushwa ulikuwa ukiniwekea vikwazo. Sasa wazee
wawili wa pale; mmoja amefariki dunia na mwingine yuko hai, wakanishauri
kuwa kwa vile wananchi wananitaka na shida yao ni kiongozi mzuri,
nihamie kwenye chama kingine. Ndiyo nikaenda NCCR Mageuzi na nikapata
ubunge.
Haya ndiyo mambo ambayo yamenifanya niingie kwenye kinyang’anyiro kwa
sababu hali inazidi kuwa mbaya. Kama hali ikiachwa hivi basi hata kwenye
urais atakayeshinda atakuwa ni mla rushwa tu na nchi itakwenda vibaya
sana.
-RAIA MWEMA: Kuna taarifa kwamba Rais mstaafu, Benjamin Mkapa,
aliwahi kutaka kukuteua kuwa mbunge wakati akiwa Rais lakini wewe
ulikataa. Kuna ukweli gani katika hili?
MAKONGORO: Katika watu ambao nawaheshimu sana kama viongozi hapa
nchini, Mzee Mkapa ni mmoja wao. Aliikuta nchi ikiwa na hali mbaya sana
lakini akaicha pazuri. Aliikuta inanuka madeni lakini akaondoka akiiacha
na akiba kubwa ya fedha za kigeni.
Sasa miezi 18 kabla hajamaliza urais wake, aliniambia anataka kuniteua
kuwa mbunge. Ni kweli kuwa nilikataa nafasi hiyo. Nilikataa kwa sababu
ingeonekana anampendelea mtoto wa Nyerere. Ingeonekana kama anatoa
zawadi. Na pengine ingeweza kujenga picha kuwa nimebebwa.
Nilikataa kwa sababu sikutaka mtu ambaye ninamuheshimu sana anyooshewe
vidole kwa ajili yangu. Nilimueleza sababu zangu na nashukuru mzee yule
alinielewa vizuri.
-RAIA MWEMA: Ni kweli kwamba baba yako, Mwalimu Julius Nyerere,
hakujua kwamba uko vitani Uganda wakati wa Vita ya Kagera hadi baada ya
vita kumalizika?
MAKONGORO: Ni kweli. Unajua mimi nilikwenda vitani nikiwa na umri wa
miaka 18 tu ambao ndiyo ulikuwa umri mdogo zaidi kuruhusiwa kwenda
vitani wakati huo.
Wakati vita inaanza mimi nilikuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kwenye Operesheni iliyojulikana kama Chakaza. Wale waliokuwa
JKT walipatiwa mafunzo kidogo na kisha kupelekwa vitani.
Mimi pia nikaenda lakini sikumwambia baba. Ulikuwa ni uamuzi wangu
binafsi. Kuna kaka zangu walikuwa jeshini tayari wakati huo lakini mimi
nilikuwa mdogo sana.
Baba alikuwa na mambo mengi ya kufanya wakati wa vita na nadhani alijua
naendelea na JKT. Kwa bahati nzuri pale nyumbani Msasani kulikuwa na
simu na baada ya vita askari tulikuwa tukirusiwa kupiga simu nyumbani.
Sasa nikaanza utaratibu wa kupiga simu nyumbani mara kwa mara kila
ilipofika saa kumi jioni. Baba alikuwa na utaratibu wa kurudi nyumbani
saa tisa na akirudi moja kwa moja anakwenda mezani ale chakula.
Baada ya muda akabaini kuwa kila saa kumi wadogo zangu wakisikia tu simu
wanakimbilia ilipo kwenda kusikiliza. Siku moja akawauliza, mbona
mnakimbilia simu kila inapofika saa kumi na saa nyingine hamkimbilii?
Ndiyo wakamwambia tunaongea na kaka Mako (Makongoro). Akashangaa,
akawaambia mnaongea naye kutoka wapi? Wakamwambia yuko Uganda. Nalisikia
alishtuka sana na moja kwa moja akaja kwenye simu.
Mara nikasikia sauti ya Mwalimu ikiuliza Uko wapi Makongoro? Nikamwambia
niko vitani Uganda? Akaniuliza uliendajeendaje? Nikamuuliza kwani
vijana wenzangu kama mimi waliendajeendaje?
Basi, nikasikia anapumua na akaanza kuniuliza kuhusu habari za Uganda na
mambo mengine. Nilikuwa sijawasiliana na baba yangu kwa muda wa miaka
miwili tangu kuanza kwa vita.
-RAIA MWEMA: Mmoja wa washindani wako kwenye kinyang’anyiro hiki
cha kuwania urais, Edward Lowassa, amewahi kuhadithia namna
alivyoshuhudia watu wakifa vitani wakati wa vita hiyo. Je, mliwahi
kukutana mkiwa Uganda?
MAKONGORO: Sikumbuki kukutana na Lowassa wakati wa Vita ya
Uganda. Lakini kulikuwa na askari wengi na inawezekana nilipokuwa mimi
yeye hakuwepo. Siwezi kujua askari wote waliopigana vita ile.
Baada ya vita kumalizika, wasanii wengi kama vile Zahir Ally Zorro
walikuja Uganda kututumbuiza lakini Lowassa pia sikumuona. Nasikia yeye
alisomea sanaa Chuo Kikuu labda alikuja wakati huo lakini pia sikumuona.
Zorro na marehemu Kapteni John Komba niliwaona wakati ule. Lakini
Lowassa sikumbuki kumuona. Labda alipigana mji mwingine au alikuja na
wasanii kutumbuiza baada ya vita, lakini mimi sikumbuki kumuona.
-RAIA MWEMA: Washindani wako wanadai kuwa wewe hufai kupewa urais kwa
sababu ni mlevi na unapenda kunywa pombe. Unazungumziaje shutuma hizi?
MAKONGORO: Mimi pombe nakunywa lakini hilo la kusema kwamba mimi
ni mlevi halipo. Mimi si mlevi. Wapo wapinzani wangu ambao ni walevi
kiasi kwamba pombe zimeharibu afya zao na sasa wanaumwa.
Wanaumwa kwa sababu ya kunywa pombe. Mimi kama unavyoniona niko fiti na
sina tatizo lolote la kiafya. Sasa wale ambao ulevi umewasababishia
matatizo hawasemwi na kibao kinageuzwa kwangu. Hiki ni kichekesho
kwelikweli.
-RAIA MWEMA: Kwa hiyo uko tayari kwenda kupimwa afya ili uthibitishe
utimamu wa afya yako kama alivyopendekeza mgombea mmoja kwamba wagombea
wote mpimwe afya zenu?
MAKONGORO: Tupimwe afya kwani tunataka kwenda kuchezea Real Madrid
au Manchester United? Wachezaji wanaotaka kwenda kucheza mpira ndiyo
wanapimwa afya zao lakini sijasikia popote watu wanaotaka urais wanaenda
kupima afya.
Kwani Watanzania hawawezi kuangalia tu wenyewe na wakajua huyu ana afya njema na yule hana?
-RAIA MWEMA: Una wito gani kwa wana CCM wenzako kuelekea kuchagua
mgombea urais kupitia chama chenu kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu?
MAKONGORO: Mimi nasema wana CCM wanatakiwa watutendee haki
wagombea, chama chao na taifa lao. Kwenye uchaguzi huu, CCM inaweza
kuamua kufanya mabadiliko chanya au hasi.
Wakichagua mtu ambaye dunia nzima inajua ni mwizi, wajue kwamba Watanzania watawaona na dunia pia itawaona pia.
Wana CCM wasibabaike na kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wagombea kwamba wasipopitishwa wao, basi patachimbika.
Sasa nauliza, patachimbika kwani kuna madini gani yanayotafutwa? CCM
imekuwa Mererani ambako wachimba madini wanachimba kutafuta Tanzanite?
Kama wana CCM watafanya makosa safari hii, wajue kwamba hawakuwa na wa kumlilia isipokuwa wao wenyewe.
source-Raia MwemaBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Home » Unlabelled » Makongoro Ammaliza Lowassa... Asema Hakumuona Vita ya Kagera, Labda alikuja baada ya vita kuisha.
Post a Comment