Zikiwa zimebaki
siku 9 kabla ya kamati kuu ya chama mapinduzi CCM akijakutana kwa ajili ya “kufyeka”
majina 37 kati ya 42 ya makada wake waliojitokeza na kuwania Urais ndani ya
chama hicho,sasa jukumu lingine lawaangukia viongozi wastaafu wa chama
hicho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Viongozi hao ambao ni marais
wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa ambao wote kwa pamoja wataunda Baraza
la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya kikao wakati wowote
wiki hii kujadili mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa Tanzania
kupitia chama hicho.
Taarifa kutoka chanzo kimoja ndani ya
CCM kimeeleza kuwa Mwinyi, Mkapa na wazee wengine wanaounda Baraza la Wazee la
Ushauri, watapasua kichwa wiki hii kujadili mwenendo wa urais ikiwa ni siku
chache kabla ya kufikia Julai 2, mwaka huu, inayoonyeshwa katika ratiba ya
uchaguzi ya CCM kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu kwa wanaowania
urais.
Lengo la kikao cha Wazee ni kujadili
kwa kina mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais na mwishowe kutoa
mapendekezo yao juu ya namna bora ya kumpata mgombea kwa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM (CC)
"Kikao hiki ni muhimu kwa hatma
ya mchakato wa uchaguzi... baada ya kutofanyika wiki iliyopita, sasa
kitafanyika wiki hii, tena wakati wowote kuanzia kesho (leo)," chanzo
kilieleza.
Mtoa taarifa huyo wa Mtandao huu ameongeza kwa kusema kuwa “hapa
sikufichi wazee hawa wanaweza kuja na mapendekezo ambayo yatakuwa magumu kwenye
wagombea ambao wamewai kukumbwa na kashfa ya Ufisadi,maana kunawagombea
wametengeneza makundi makubwa kwenye chama chetu tena makubwa sana na Busara
hizi za wazee zinaweza kuwaweka wagombe wenye Kashfa kubwa”amesema
Makada hao wa CCM ambao wanawakati mgumu ni Waziri mkuu aliyejiuzelu
kwenye Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni tata ya kufua umme ya Richmound,Edward
Lowassa pamoja na Waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye anathumumiwa kwa kitendo
chake cha kufumbia macho uporaji wa Mabilioni ya Fedha kwenye Akaunt ya Tegeta
Escrow.
Awali, kikao hicho kilitarajiwa
kufanyika Jumatano iliyopita jijini Dar es Salaam lakini kikaahirishwa na
Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee, Pius Msekwa, kutokana na kile
kilichoelezwa kuwa ni baadhi ya viongozi wakuu wa CCM kuwa safarini.
Alipoulizwa na chanzo changu jana
iwapo watakutana kaunzia leo, Msekwa hakuwa tayari kueleza kiundani na badala
yake alimjibu mwandishi kwa kifupi: "Just pay attention (wee jiweke tayari
tu) kama umesikia juu ya kikao chetu."
Kikao cha Baraza la Ushauri la Wazee ni
mahususi kwa ajili ya ushauri juu ya watia nia 42 wa urais waliojitokeza kutaka
kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge
na madiwani utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Wanaounda baraza la wazee
Wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee
kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanywa na CCM mwaka 2012 katika katiba yake ni
marais wastaafu Mwinyi (Mwenyekiti), Mkapa (Mjumbe), Amani Abeid Karume
(Mjumbe) na Dk. Salmin Amour (Mjumbe).
Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu na
Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela (mjumbe) na Pius Msekwa (Katibu).
Mkutano huo wa Baraza la Wazee CCM ni
utangulizi wa mfululizo wa vikao vingine vya chama hicho vitakavyoanza Julai 5,
mwaka huu.
Vikao vingine ambavyo viko katika
maandalizi ya kukutana ni Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa
itakayokutana Julai 7 na Kamati Kuu (CC) itakayokutana Julai 8, chini ya Rais
Kikwete, ikifuatiwa na kikao cha NEC Julai 9, mwaka huu.
Post a Comment