Loading...

EXCLUSIVEE.......ZITO KABWE AMLIPUA TENA EDWARD LOWASA USIKU HUU...HII SASA BALAA

BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
 http://www.itv.co.tz/media/image/kabwe11.jpg

Nilihoji wagombea 4 uhusika wao kwenye masuala mbalimbali. Prof. Mwandosya na Ben Membe wamejibu. Lowasa na Magufuli bado. Sehemu ya Hotuba yangu hii

Lindi 26.06.2015

1) Edward Lowasa hanabudi kuwaeleza Watanzania kwa ufasaha kuhusu tuhuma zake katika mchakato wa manunuzi ya kampuni ya kufua Umeme ya Richmond. Mradi huu wa dola 172 milioni ndio uliopelekea yeye kujiuzulu Uwaziri Mkuu. Ndio anasema aliwajibika kwa makosa ya waliochini yake lakini anataka nafasi kubwa sana na yenye nguvu kubwa. Hivyo bila kuelezea uhusika wake katika suala hili wananchi wa Tanzania hawatatendewa haki kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Pia ametamka kuwa yeye ni tajiri na anachukia umasikini lakini hajaeleza utajiri huo ameupataje, ana miliki Mali kiasi gani na ana hisa kwenye kampuni zipi za kibiashara. Habari za chini chini zinasema pia yeye ndiye alikuwa na zabuni ya kusambaza mabomba kwenye mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwenda mji wa Kahama akiwa Waziri wa Maji na Mifugo. Edward Lowasa hana budi kuyaweka haya wazi umma ujue.

2) Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali. Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International. Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

3) John Pombe Magufuli anasifika katika uchapa kazi ingawa hajawahi kuonekana waziwazi kwenye mapambano dhidi ya rushwa. Kwenye kashfa nyingi zilizopata kutokea nchini msimamo wa Magufuli haujulikani alisimama upande upi. Wananchi wana haki ya kupata majibu kutoka kwa Bwana Magufuli kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali. Uporaji mkubwa zaidi wa Mali za nchi kuwahi kutokea katika nchi yetu ni uuzwaji wa nyumba za Serikali. Waziri Magufuli alituhumiwa kwa kuuza nyumba kifisadi kiasi cha hata wadogo zake na watu wengine wasio watumishi wa umma. Wananchi lazima wapate majibu ya mambo haya.

4) Benard Camilius Membe amekuwa akijaribu kuzungumzia ufisadi na nia yake ya kupambana na ufisadi kila apatapo nafasi ya kuzungumza. Hata hivyo anapaswa kuelezea tuhuma dhidi yake kuhusu fedha zaidi ya dola za marekani 20 milioni za mkopo uliorekebishwa kutoka Libya. Suala hili limekuwa likisemwa chini chini na hivyo membe mwenyewe kulipotezea lakini ni jambo lenye kuhitaji Maelezo ya kina kabisa. Msaada huu ulikuwa uwekezwe kwenye kiwanda cha Simenti mkoani lindi ili kuongeza uzalishaji wa simenti nchini na kuongeza ajira kwa Watanzania. Je kiwanda kimejengwa? Je ndugu Membe anahusika vipi na tuhuma hizi kuhusu fedha za Libya? Kwenye nchi zenye misingi thabiti ya uwajibikaji Waziri Membe alipaswa kuwekwa kikaangoni na Bunge kueleza jambo hili. Kwa kuwa anagombea Urais ni muhimu alisemee.

Mifano hii ya wagombea 4 wa CCM inaonyesha dhahiri kwamba nchi yetu inahitaji kuelekeza vita dhidi ya ufisadi kwa kujenga taasisi imara na madhubuti za uwajibikaji. Vinginevyo vita dhidi ya rushwa na ufisadi inakua ni porojo tu za wanasiasa. Wote tuliowainisha hapo juu wamesema katika hotuba zao za kutia nia kuwa watambana na rushwa. Hakuna aliyesema atapambana vipi na rushwa na ufisadi. Hakuna aliyethubutu kutamka neno Miiko ya Viongozi. Hakuna aliyethubutu kusema ataweka wazi Mali, Madeni na Maslahi yake.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT WazalendoBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWS TIME | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top