BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Dar
es Salaam. Kauli ya Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ya kutaka
wajumbe wa Halmashauri Kuu kupiga kura na wale wasioafiki watoke, ndiyo
inaelezwa kuwa ilimaliza mzozo ulioibuka baada ya jina la Edward Lowassa
kuenguliwa mapema.
Kikao
hicho kilichofanyika Julai 10 kilionekana kuelekea kukumbwa na
mtafaruku baada ya wajumbe kumpokea Rais Jakaya Kikwete kwa wimbo wa
kuonyesha kuwa wana imani na waziri huyo mkuu wa zamani ambaye jina lake
halikuwamo miongoni mwa makada watano waliopitishwa na Kamati Kuu ya
CCM.
Habari
ambazo Mwananchi imezipata kutoka kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu
zinasema kuwa baada ya mapumziko ya chakula cha mchana, ulizuka mjadala
mkubwa kuhusu kuenguliwa kwa Lowassa, ambaye alionekana kuwa alikuwa
akiongoza mbio za urais ndani ya chama hicho.
Habari
hizo zinasema wakati wa mjadala huo ndipo wajumbe wa Baraza la Ushauri
la Viongozi walipoingilia na kuanza kutoa ushauri mmoja baada ya
mwingine kabla ya Mkapa kuzungumza na baadaye kusema “twendeni tukapige
kura, asiyetaka atoke”, ndipo hali ya ukimwa ilipotanda na kufuatiwa na
kazi ya kupiga kura iliyoashiria kuwa amani imerejea.
Hata
hivyo, haikuwa rahisi kwa kikao hicho chenye wajumbe takriba 400
kutulizwa na kufikia hatua ya kupigia kura majina matano ili kupata
matatu ambayo yalipelekwa kwenye Mkutano Mkuu.
Habari
ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa wajumbe waliokuwa wakimtaka
Lowassa walikuwa wakihoji sababu za mbunge huyo wa Monduli kuenguliwa
huku jina la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe likiachwa.
Alikuwa
mwenyekiti wa baraza hilo, Ali Hassan Mwinyi aliyeanza kwa kuwaeleza
wajumbe historia ya changamoto zilizokipata chama hicho, aliyoyaona
mwaka 1995 wakati kulipokuwa na wagombea 17, lakini walioingia kwenye
mchujo walikuwa 15, wakiwemo Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Cleopa
Msuya.
Mwinyi
aliwashauri wajumbe kuwa kama wanampenda mtu, wawe na kiasi na kama
wanamchukia mtu, wawe na kiasi pia na kwamba wasifanye mambo hayo kwa
kupitiliza kwani matokeo yatapokuwa tofauti na walivyotarajia wao ndiyo
wataathirika zaidi kuliko muhusika.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa mwingine aliyetoa nasaha zake alikuwa Waziri
Mkuu wa zamani, John Samuel Malecela, ambaye aliimbia kwenye mbio hizo
mwaka 2005 wakati walipojitokeza makada 11 kuwania kuteuliwa na CCM.
Malecela,
ambaye wakati huo alikuwa na wadhifa wa makamu mwenyekiti wa CCM Bara,
Malecela aliwaeleza wajumbe hasa walikuwa na mapenzi na Lowassa kwamba
hata yeye wakati huo alikuwa na kundi kubwa la watu waliokuwa wanamuunga
mkono kutoka Kanda ya Ziwa.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa, Malecela aliwaambia wajumbe wa NEC kwamba
wafuasi wake walikuwa wakilia kwa uchungu kutokana na jina lake kukatwa,
walimshauri mengi ikiwemo ya kuhama chama, lakini aliwaambia “chama
kwanza mtu baadaye”, kwa maana huo ndiyo ulikuwa uamuzi wa chama na
unapaswa kuheshimiwa.
Wakati
huo, baada ya Rais Kikwete kutangazwa kuwa ndiye ambaye angepeperusha
bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, alikwenda kumpa mkono
wa hongera na kuahidi kumuunga mkono.
Mjumbe
mwingine wa baraza hilo, Amani Abeid Karume, ambaye alikuwa Rais wa
Zanzibar, anasemekana kuwa aliwaambia wajumbe kwamba wafanye mambo kama
watu wazima, kwa kuwa kuna mambo ya mtu yanaweza kuzungumzwa hadharani,
lakini kuna mengine yanahitaji staha ili kuepuka kudhalilishana.
Aliwashauri
wajumbe wasipende kutaka kila kitu cha mtu wanayedhani anaonewa kiwekwe
wazi kwa kuwa kuna mengine hayastahili kuwekwa hadharani, na
kuwasisitizia kufikiri kama watu wazima.
habari
hizo zinasema kuwa aliyebadilisha kabisa mwelekeo wa kikao alikuwa Rais
Mkapa ambaye aliwaeleza wajumbe kwamba mambo yote wanayozungumza kuhusu
uonevu siyo sahihi kwa sababu mwenyekiti wa chama, Rais Kikwete ana
taarifa kuliko wao kwa kuwa anazo nyenzo za kumpatia taarifa na namna ya
kuzithibisha ukweli wake.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa Mkapa baada ya kusema maneno hayo alisema: “Twendeni tukapige kura, asiyetaka atoke.”
Maneno
ya wazee hao na hasa ya Mkapa yaliwanyong’oneza wajumbe hasa waliokuwa
wakipinga uamuzi wa Kamati Kuu, na baada ya hapo hakuna aliyeinua kinywa
chake kutaka kuzungumza kitu au kupinga jambo.
Kikao
hicho kilikuwa na usiri mkubwa baada ya wajumbe kuzuiwa kuingia na simu
kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za makao makuu ya CCM, White House
uliopo katikati ya mji wa Dodoma.
Baraza
la Ushauri linaoongozwa na Rais Mwinyi (mwenyekiti), katibu wake ni
Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa, wakati wajumbe ni marais
wastaafu, Mkapa, Karume, Dk Salmin Amour na Makamu wa Rais wa Pili na
Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela.
Wastaafu
hao walikuwepo kwenye vikao vyote, na Malecela, ambaye alikuwa London
nchini Uingereza, aliwasili siku ya kikao cha Kamati Kuu, na kwa umuhimu
wake alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alikuta
ndege nyingine ikimsubiri uwanjani hapo kwa ajili ya kumpeleka Dodoma.
Dalili
za kuzuka mtafaruku kwenye kikao cha Halmashauri Kuu zilianza mapema.
Wakati Mwenyekiti akiingia na viongozi wengine, wajumbe walianza kuimba
wimbo wa “tuna imnani na Lowassa”, badala ya maneno yanayotumika kwenye
wimbo huo ambao hupachikwa jina la mwenyekiti wa chama.
“Haijapata
kutokea,” alisema Rais Kikwete baada ya kukaa kwenye kiti na kuongeza
kuwa mambo yote yatazungumzwa taratibu na muafaka utafikiwa.
Mtoa
taarifa wetu anasema kuwa Rais Kikwete alikuwa mvumulivu, akitoa mwanya
kwa wajumbe wengi kuzungumza licha ya baadhi kumshambulia wakidai
familia yake inampigia kampeni Membe.
Habari zinasema pamoja na shutuma zote hizo, Kikwte hakujibu hoja hizo zaidi ya kutoa mwanya kwa wajumbe wengi zaidi kuchangia.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa ilifika wakati wajumbe wakaanza kushambuliana
wao kwa wao, huku wengine wakisema hawajaenda humo kujadili jina la mtu
mmojBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment