Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.
Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi
Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.
Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.
Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.
Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.
Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.
Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.
Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.
Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??
Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.
CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.
Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyeweBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Post a Comment