BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE
TAIFA Edward Lowassa ni balaa kwa Taifa! Democratic Party (DP)
inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake
sita, Edward Lowassa na wengine, kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya
Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za
Nchi kwa kuanza kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu
wa Sheria.
1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowassa na
wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati,
na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12.
Lakini safari hii Lowassa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano
mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!
2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama
chake, katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na
Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowassa amefanya
mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano
wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii
ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi!
Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue
mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi, kiasi
kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini, upelelezi wa
Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata
ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi
Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani, kumehusika ‘’Money
laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama
mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa. Ni
marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea
urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za
Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni
maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa
Sheria
4 Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia
kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya
mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi
nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara
kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa
sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa
kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi
yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi! Kwa
kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha
kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo
kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!
5 Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu
siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia
maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi
uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6 Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa sababu
alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote
aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na
kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua mvua
Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa
ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi.
Ni mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga
Lowasa, anayeweza kumruhusu fisadi Edward Lowassa agombee urais. Sifa za
mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika
Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo!
Lowasa awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama
“Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi
papa, kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika
kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond,
lakini leo akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!
Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh
Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward Lowasa! Si
ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa
yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na
mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji
Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV
yake.
Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake
wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi kama
China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa
risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais! Kwa
ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima
mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila
mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha
kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:
a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima
viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji
wa akili zake.
c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea
wananchi wote kila walipo, na kusimamia utekelezaji wa majukumu yote ya
watendaji wote katika Taifa, hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na
afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote
d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na
kusababisha maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa.
Na udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi
mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya
kupoteza uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii
yake atatumikia maslahi yake zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya
likawa limelikosesha Taifa kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!
e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu
za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa Taifa, hususan
ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na
umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu,
kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa
kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya afya bora, ambayo ni
ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa dhamana kubwa sana ya
kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta
kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya
maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya anagombea asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli
tunalithamini na kuliheshimu Taifa. Sifa za urais ni wito au uhanga kwa
ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na
AFYA BORA.
Ni dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa
watu! Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili
umati wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’.
LOWASA NI MOJAWAPO WA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU WA;IOKUWA WANATIBIWA NA
BABU WA LOLIONDO NA TANGIA PALE HAJAPONA NA ZAIDI SANA ANAANZA
KUTETEMEKA
Source: Mtikila Mwenyewe :0766 053081 KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU.docxBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...
Post a Comment