MNAMO MWAKA 2008 JOHN MNYIKA ALIANDIKA KATIKA MTANDAO WAKE HIVI "SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASA" LAKINI KITU CHA AJABU LEO HII WAMEMKARIBISHA MTU AMBAYE YE MWENYEWE ALIMWANDIKIA HUU WALAKA
Hebu usome hapa chini alivyo uandika mnyika kipindi hicho
Wednesday, September 3, 2008
SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA
Siku chache zilizopita.
Nilitoa taarifa hii kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, kwa sababu ambazo
sizifahamu, habari hii haikutoka katika magazeti mengi ya kila siku.
Pengine inaweza ikawa ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe(barua pepe)
lakini kuna uwezekano mkubwa sababu ikawa ni kuwa Lowassa hakutajwa
kuchukuliwa hatua kama hizi ambazo nimezieleza hapa katika yale Maazimio
23 ya Bunge. Yeye aliambiwa tu atakafakari na kuchukua maamuzi ambayo
ataona yanafaa. Yeye akaamua kujiuzulu. Lakini bado siridhiki sana na
sababu hii kwa kuwa maazimio hayo 23 hayajasema Karamagi na Msabaha
wachunguzwe kuhusu Rushwa kama serikali ilivyoamua. Kama imeamualiwa na
Serikali hawa wachunguzwe, kwanini serikali haikumjumuisha na Lowassa?
Hii inafanya niamini kwamba bado msimamo huu hapa chini ni mwafaka:
TAARIFA KWA UMMA
SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA
- Ni mmoja wa mizizi ya ufisadi wa Richmond
- Akamatwe, ahojiwiwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Tarehe
25 Februari, 2008 Vijana wa CHADEMA tulitoa taarifa kwa umma tukikemea
jitihada zilizokuwa zikiendelea za Lowassa kujisafisha na kusafishwa na
tukahimiza achukuliwe hatua za haraka kutokana na tuhuma za ufisadi
na/ama matumizi ya madaraka katika kashfa ya RICHMOND. Pamoja na taarifa
yetu hiyo kwa umma katika kipindi chote ambacho Serikali ilipewa na
Bunge kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo hatua
tulizopendekeza hazikuchuliwa. Aidha tumefadhaishwa zaidi na Taarifa
ambayo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo ameiwasilisha Bungeni Alhamisi 28
Agosti, 2008 pamoja na kutaja hatua ambazo zimechukuliwa kuhusu
watuhumiwa wengine ikiwemo kuandikiwa Barua za kujieleza na/ama kuanza
kuchunguzwa na vyombo vya dola/usalama; Waziri Mkuu hakueleza hatua
ambazo zimeaanza kuchukuliwa dhidi ya Bwana Lowassa.
Tunatambua
kuwa Waziri Mkuu katika taarifa yake ameeleza kuhusu hatua ambazo
serikali imeanza kuchukua ikiwemo za marekebisho ya Sheria ama mifumo ya
uwajibikaji, ikiwemo ile ya manunuzi. Hata hivyo, tungependa kuweka
bayana kwamba matatizo ya msingi ya taifa letu hayasababishwi na
mapungufu katika sheria pekee, ila kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na
kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa
viongozi. Hivyo, tunapenda kuwajulisha Watanzania kuwa kama watuhumiwa
wa ufisadi hawatachukuliwa hatua mapema, misingi ya utawala wa sheria
itazidi kutetereka na matokeo yake ni kuwa mageuzi yoyote katika mifumo
ya kiutawala hayatatekelezwa kikamilifu. Kwa ujumla tunaamini kwamba
utamaduni huu wa kulindana katika serikali unatoa mfano mbaya kwa vijana
wa kitanzania kuhusu uongozi na utawala bora.
Tungependa
kusisitiza kuwa Bwana Lowassa, akiwa Waziri Mkuu wa nchi yetu wakati
huo alikuwa mmoja wa mizizi mikuu ya ufisadi wa RICHMOND. Hivyo, tunaona
kuwa Taarifa ya Utekelezaji ya Waziri Mkuu Pinda imejikita katika
kushughulikia matokeo badala ya mzizi wa tatizo lenyewe na hivyo kama
hali hii ikiendelea itaporomosha nidhamu na uwajibikaji katika taifa
letu. Tunaamini kwamba kama Bwana Lowassa aliyekuwa kinara wa Serikali
wakati huo, ataweza kuchukuliwa hatua kikamilifu basi itakuwa rahisi kwa
waliokuwa chini yake kuweza kuchukuliwa hatua za haraka na hatimaye
kurejesha maadili katika utawala. Lakini kama Serikali itaendelea
kumlinda Bwana Lowassa na kuwatoa kafara maafisa wa chini, bado
haitakuwa imetekeleza kikamilifu dhana ya uwajibikaji na utawala wa
Sheria. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na mawaziri wenzake kadhaa ni hatua
ndogo sana katika kashfa iliyohusisha uvunjaji wa Sheria za nchi yetu,
mazingira ya ufisadi na hasara kubwa kwa taifa.
Sisi
tunaona kutotajwa kikamilifu kwa hatua zilizochuliwa juu ya Bwana
Lowassa ni mwendelezo wajitihada za miezi ya karibuni za Bwana
Lowassa(Mb) kupita akijitetea kuanzia katika hotuba yake alipokwenda
Jimboni Monduli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na hata
mahojiano yake maalumu na Televeshioni ya Taifa(TVT).
Aidha,
taarifa ya Waziri Mkuu Pinda imeakisi uamuzi wa Waziri Mkuu
aliyejiuzulu Bwana Edward Lowassa kujitokeza miezi ya karibuni kujitetea
kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond ambayo kwa ujumla ni
ishara ya unafiki wa kisiasa. Itakumbukwa kuwa baada ya Kamati Teule
kuwasilisha taarifa yake, Bwana Lowassa alipata nafasi bungeni takribani
mara mbili kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni wakati akiwa
Waziri kuzungumzia suala hili lakini hakutoa utetezi ambao Mwezi
Februari alijaribu kuutoa kwa umma. Waziri Mkuu Pinda inabidi auleze
Umma kama uamuzi wa kumtomtaja katika Taarifa yake ya utekelezaji kuhusu
hatua ambazo amechuliwa ni ishara kuwa serikali imekubaliana na utetezi
wa Bwana Lowassa.
Itakumbukwa
kuwa Vijana wa CHADEMA tulieleza wazi kwamba katika kujitetea kwake
mwezi Mei, Bwana Lowassa alithibitisha wazi uzembe na matumizi mabaya ya
madaraka ambayo aliyafanya alipokuwa Waziri Mkuu wakati wa sakata zima
la Richmond. Hivyo, tunarudia kutoa mwito kwa vyombo vya dola kuweza
kumkamata, kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria dhidi ya uzembe na
matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Badala ya Bwana Lowassa kuendelea kupita akijitetea kuwa Kamati Teule
haikumuita kuweza kujieleza; vyombo vya dola vimkamate akatoe maelezo
yake panapohusika. Vyombo vya dola vimekuwa vikiwakamata raia wa kawaida
wenye taarifa za uhalifu kuweza kuisadia polisi, inashangaza Bwana
Lowassa amejieleza wazi kuwa alikuwa anafahamu uhalifu uliokuwa
ukitendeka lakini bado yuko nje akijitetea na pia Taarifa za kiserikali
zikielekea kumlinda. Tunaamini akikamatwa yeye, atawezesha watuhumiwa
wakuu wa kashfa ya Richmond kuweza kupatikana. Tulieza wazi katika tamko
letu na Mwezi Februari kuwa , jitahada zozote za kumlinda na kumtetea
zingeweza kuathiri mwekekeo wa hatua ambazo zitanatarajia kupendekezwa
na Kamati ya Waziri Mkuu mpya Mheshimiwa Mizengo Pinda. Kutokana na
Taarifa ya Waziri Mkuu Pinda aliyowasilisha Bungeni Alhamisi tarehe 28
Agosti, 2008 ni wazi kuwa kuna kila dalili kuwa mwelekeo huo umeanza
kuathiriwa, hivyo tunarudia tena kutaka Bwana Lowassa achukuliwe hatua
kabla ya Bunge la Mwezi Novemba, 2008.
Bwana
Lowassa akiwa Waziri Mkuu amethibitisha kwamba maneno yake mwenyewe
kuwa alikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na
Sheria ya Makosa ya Udhibiti wa Uhujumu wa Uchumi wa nchi ya Mwaka 1984.
Bwana
Lowassa alikiri kwamba alikuwa anafahamu kwamba Richmond ni kampuni ya
kitapeli, lakini katika kipindi chote cha uongozi wake aliinyamazia hali
hii na kwa kiasi kikubwa aliitetea kampuni hiyo mbele ya macho ya umma.
Wakati wa Viongozi mbalimbali wa upinzani walipoweka bayana kwamba
Richmond ni kampuni isiyo na uwezo, serikali ilitetea kampuni hiyo.
Vyombo mbalimbali vya habari vilimtuhumu Bwana Lowassa mwaka 2006 na
2007 kama kiongozi wa Shughuli za serikali bungeni, kwamba alishiriki
‘kuwaziba midomo’ wabunge wa CCM wasijadili suala hili. Pia, ni Bwana
Lowassa huyo huyo, alinukuliwa akiwa Arusha akiwataka watanzania
wasiijadili kampuni ya Richmond baada ya mvua kuanza kunyesha. Kama
Bwana Lowassa wakati wote huo alijua kama ni kampuni ya kitapeli kama
anavyojaribu alivyojaribu kujitetea, uamuzi wake wa kuwaasa watanzania
wasiijadili ulikuwa ni wa kulinda ufisadi ambao aliufahamu. Inashangaza
pia ni Lowassa huyo huyo alisema alijua kuwa Richmond ni kampuni ya
kitapeli; ni Lowassa huyo huyo alisema kwamba alishauriwa vibaya na
watumishi wa umma aliowataja kuhusu uwezo wa Richmond; Ni Lowassa huyo
huyo aliyesema kwamba alijua kuwa TANESCO chini ya Menejimenti ya Net
Group Solution walitaka kuhujumu mchakato wa tenda na hivyo
‘kuwanyang’anya’. Lakini ni Lowassa huyo huyo aliyekuwa Waziri Mkuu
ambaye angeweza kuviagiza vyombo vya dola kumwezesha kuthibitisha
‘utapeli wa Richmond’; hivyo, maelezo ya sasa yanayotolewa kuhusu
ushiriki wake yanaonyesha kuwa sasa kuna mwelekeo wa kumlinda.
Tunaendelea
kushangazwa na Serikali na Bwana Lowassa kutumia utetezi wake kueleza
tu nia yake ya kutaka mkataba wa Richmond usitishwe; nia ambayo kama ni
kweli alikuwa na uwezo wa kuitekeleza na hakuitekeleza. Tunaitaka
Serikali na Bwana Lowassa kuweka bayana ni kwa vipi Richmond ilipewa
tenda hiyo na kwa shinikizo la nani. Bwana Lowassa anakwepa
kuyazungumzia haya kwa kuwa anajua kabisa kwamba ni yeye aliyetumia
madaraka yake vibaya alipokuwa Waziri Mkuu kwa kukiuka Sheria na
Taratibu za Ununuzi kwa ‘kupora’ mchakato uliokuwa ukiendeshwa na
TANESCO, ‘kuunda kamati yake’ na kuzisukuma mamlaka za ununuzi hali
iliyopelekea Richmond kupewa tenda ili hali haikuwa na uwezo uliotakiwa.
Ni uzembe huu ambao umelisababishia hasara taifa kwa kulipa shilingi
milioni 152 kila siku kwa kampuni ya Dowans
iliyohamishiwa mkataba wa kitapeli wa Richmond; na takribani bilioni 172
kwa ujumla ambazo taifa linawajibika kuzilipa kutokana na kukodisha
mitambo hiyo. Hvyo tunarudia tena rai yetu ya
kutaka fedha zilizozilipwa kizembe mpaka sasa kurejesghwa serikalini.
Kwa vyovyote vile, jitihada za Bwana Lowassa za kuhamasisha ujenzi wa
Sekondari Kata, na utumishi wake kama Waziri Mkuu katika kipindi cha
miaka miwili, haviwezi kuzidi hasara aliyosababisha katika uchumi wetu
kipindi chote tulichokosa umeme wa dharura na wala hailingani na hasara
ambayo tunaendelea kuilipa kila siku iendayo kwa Mungu. Maamuzi haya ya
Bwana Lowassa yanaendelea kuwaumiza wananchi wote ikiwemo wa Jimbo lake
la Monduli ambao wanataabika kwa mzigo wa gharama za umeme.
Tunarudia
tena kumkumbusha Rais Kikwete kwamba Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa
zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa
viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali
na katika sekta ya umma. Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile
imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye
huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili
ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.
Kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao
kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma. Hivyo, taarifa ya Waziri
Mkuu Pinda kutokueleza bayana hatua ambazo Bwana Lowassa ameshachukuliwa
au atachukuliwa ni ishara kuwa kauli ya Rais
Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na Wazee wa CCM mkoani Dar es
Salaam kwamba Bwana Lowassa amepata tu ‘ajali ya kisiasa’, na kumsifu
kwa utumishi wake imechangia kumlinda mhusika huyu mkubwa katika sakata
zima la RICHMOND. Vijana wa CHADEMA tulitarajia kuwa, baada ya Bwana
Lowassa kukiri mwenyewe hadharani kuhusu uzembe wake na matumizi mabaya
ya madaraka Rais Kikwete angelekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yake
badala ya kuendelea kumpamba kama “shujaa wa uwajibikaji’, kinyume na
hayo tutaamini kwamba serikali yake inaendeshwa kwa ‘ubia wa kulindana’.
Aidha tunarudia kutoa rai kwamba Rais Kikwete kuwafukuza kazi watumishi
wote wa umma waandamizi ambao wametajwa na Bwana Lowassa kushiriki
uzembe na matumizi mabaya ya madaraka; watumishi ambao walitajwa pia na
Kamati Teule ya Bunge lakini mpaka sasa wanaendelea kutumikia nafasi zao
mbalimbali. Kwa kuwa Waziri Mkuu Pinda ameshatangaza kwamba kwa wale
wateule wa Rais, Kamati yake imeshapeleka suala zima kwake, tunategemea
Rais atachukua hatua za haraka ili kuonyesha mfano kwa viongozi wengine
wa chini yake wanaotarajiwa kuchukua hatua kwa watumishi wa chini.
Kadhalika
tunapenda kuvikumbusha tena vyombo vya dola kwamba Sheria ya Udhibiti
wa Makosa ya Kuhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo
kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi ni pamoja na yale yote yenye
kusababisha hasara kwa mamlaka ya Serikali. Pia Sheria
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inatamka kuwa
ubadhirifu na/au ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na watumishi wa umma
na Matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi, ni sehemu
ya ufisadi. Bwana Lowassa alithibitisha kwamba maneno yake kwamba wapo
viongozi waandamizi wa Serikali ambao amewataja kwa majina wamefanya
maamuzi ya kifisadi, kitendo chake cha kunyamazia ufisadi huo- kinafanya
iwe vigumu kwa yeye kutenganishwa na tuhuma za ufisadi zilizomo katika
mchakato mzima wa kupewa tenda kwa kampuni ya Richmond na mambo yote
yaliyotokea baada ya Mkataba huo kuhamishiwa kwa kampuni ya Dowans.
Aidha
tumefadhaishwa na Taarifa ya Waziri Mkuu Pindi kwamba kujiuzulu kwa
Waziri Mkuu na Baadhi ya Mawaziri ilikuwa ni ishara ya hatua ambazo
serikali imechukua kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala husika.
Tunarudia kukumbusha kwamba toka sakata la Richmond lilipoanza zaidi ya
mwaka mmoja uliopita tulimtaka Bwana Lowassa kujiuzulu kulinda heshima
yake lakini alikaidi na kuitetea kampuni ya Richmond. Uamuzi wa yeye
kujiuzulu baada ya kashfa yote kuwa hadharani, umesaidia tu kuilinda
serikali ya CCM lakini katu hauwezi kumpatia heshima ya uwajibikaji na
wala hakuwezi kuwa ishara ya kwamba Maazimio ya Bunge yameshatekelezwa.
Kwa
niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), kwa taarifa hii
tunarudia kukemea jitihada zozote za kumlinda na kumtangaza Lowassa kuwa
shujaa katika taifa letu kwani hali hii ikiachwa kuendelea inatoa mfano
mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote katika
taifa letu, mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya
mafisadi(list of shame) kulindwa na kuenziwa kama shujaa wa Taifa letu
kwani ni kuharibu maana nzima ya ushujaa katika uwajibikaji.
“Inasikitisha
kwamba vijana wezi wadogo wadogo wakijazana magerezani. Vijana
wamachinga kuendelea kukosa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara;
wanafunzi wa elimu ya juu wakipandishiwa ada na wengine kukosa mikopo-
huku fedha za walipa kodi zikiendelea kuteketea kwa ufisadi na
watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kutamba hadharani. Hali hii ikiachwa,
itaharibu utawala wa sheria na kuleta matabaka katika taifa letu. Vijana
tusingependa kuona nchi yetu inatumbukia kwenye migawanyiko kwa sababu
ya kuwalinda watu wachache kwa kisingizio cha haki za binadamu”
Imetolewa tarehe 31 Agosti 2008 safirini Kenya na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553SOURCE - http://mnyika.blogspot.com/2008/09/serikali-iache-kumlinda-lowassa.html BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
1 comments:
hhizo kejeli,mwito kwamba nikamatwe vyote nimeviona na kwamba washirika wangu wa sasa ndio watuhumu wakuu,mm kama kiongozi wenu wa ukawa namuomba mungu anipe kura nyingi ktk uchaguzi mkuu,li baadae nije nichukue hatua mahsusu kwa wale wote waliohusika kinibatiza majina yasiosimilka vitabuni.mwenyezi mungu nisaidie.fisadi
ReplyPost a Comment