BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amehitimisha ziara yake ya kutafuta
wadhamini katika Mkoa wa Morogoro huku kada mkongwe wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu Issack Mwisongo, akisema Baba wa Taifa
hayati Mwalimu Julius Nyerere, hakuwahi kutamka kumkataa mbunge huyo wa
Monduli kama ambavyo baadhi ya viongozi wanasema.
Katika Mkoa huo ambao ni wa 31, Lowassa alipata wanachama 104,038 waliomdhamini.
Kanali Mwisongo alisema tangu alipojiunga na Tanu mwaka 1967 ambayo sasa
ni CCM, hajawahi kumsikia hayati Mwalimu Nyerere akitamka neno la namna
hiyo na amekuwa akihudhuria vikao vyote kuanzia Halmashauri Kuu ya CCM
(Nec), Kamati Kuu na Mkutano Mkuu.
“Mimi nimekuwa katika vikao hivyo vyote na kama Nyerere ukikosea au
hakutaki, alikuwa anakukataa waziwazi na pia unatangazwa kwenye vyombo
vya habari. Lowassa ni mtu anayewapenda Watanzania tangu zamani,”
alisema Kanali Mwisongo.
Alitolea mfano wa mwekezaji aliyedai kuwa aliletwa na mmoja wa `wakubwa '
ili ajenge hoteli katika chanzo cha gesi, lakini Lowassa aliyekuwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa wakati huo, alikataa.
“Alikataza hoteli kujengwa katika chanzo cha gesi kwa manufaa ya
Watanzania na kila alichoamua aliamua kwa manufaa ya Watanzania,”
alisema Kanali Mwisongo.
Aidha, aliwaonya viongozi wa chama hicho kuacha kutoa matamshi kabla ya
vikao havijakaa kwani ni makosa makubwa na wanasababisha CCM kuyumba
kama hakina mwenyewe.
“CCM kimeyumba kupita kiasi kutokana na hawajui msemaji mkuu ni nani na
vikao vikuu vinakaa saa ngapi vya kuamua hayo yanayosemwa ovyo. Viongozi
wasifanye makosa katika Kamati Kuu, Kamati ya Maadili ambako kutakuwa
na mizengwe, lakini watambue Nec ina nguvu,” alisema Kanali Mwisongo.
Naye Kada mwingine mkongwe, Dk. Juma Ngasongwa, ambaye amewahi kuwa
Waziri katika awamu mbalimbali, alisema viongozi wa CCM wameyumba siku
za karibuni kutokana na kusemana hadharani wenyewe kwa wenyewe na
Lowassa ndiye dawa ya kuondoa maneno hayo.
“Kuna wanachama wengi wamehamia vyama vingine kutokana na kushindwa
kuongoza CCM. Sasa huko katika vyama vingine watawezaje kuviongoza? CCM
irudishe wana-CCM imara madarakani ambaye ni Lowassa,” alisema Dk.
Ngasongwa.
Kwa upande wake, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven
Mashishanga, alisema vikao vinavyotarajiwa kukaa hivi karibuni
vihakikishe vinatenda haki kwa kuangalia ni nani aliye na alama nyingi
za vyema mgongoni na anayehitajika na wengi.
Alisema Lowassa ni kiongozi pekee mwenye uwezo na sifa za kuwa Rais kwani amekitumikia chama kwa miaka mingi.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, alimtaka
Nape Nnauye, kuacha kutoa kauli kuwa wananchi wengi wamepewa fedha kwa
ajili ya kumdhamini Lowassa wakati wapo wagombea wengi wamefika kuomba
udhamini na kutoa rushwa.
Alisema hakuna mtu aliyepewa fedha kwa ajili ya kumdhamini Lowassa, bali
ni wananchi wenyewe ndiyo wana maamuzi ya mwisho ya kumchagua kiongozi
wanayemtaka na si Nape.
“Haki isipotendeka katika vikao vya maamuzi sisi bado tupo pamoja na
wewe, katika semina ya wenyeviti tuliyopewa tuliambiwa tuchague viongozi
wanaokubalika ndani na nje ya Chama ambaye ni wewe,” alisema Juma.
Akizungumza na wanachama CCM, Lowassa aliwashukuru kwa kumdhamini na kwamba Mkoa wa Morogoro amepata watu wengi.
Hata hivyo, alisema licha ya kupata wadhamini wengi, atapeleka
wanaotakiwa CCM na wengine atawahifadhi nyumbani kwake kama kumbukumbu
yake.
Lowassa amepata jumla ya wadhamini 863,479 katika mikoa 31 aliyoitembelea.
Aidha, alitaja sababu za kugombea urais kuwa ni pamoja na kuchoshwa na
hali ya umaskini na pia Rais Jakaya Kikwete, anamaliza muda wake wa
uongozi hivyo anatakiwa kukabidhi kijiti kwa mtu mwingine.
"Na anayeweza kukipokea kijiti hicho na kuyaendeleza yale aliyoyaacha
Rais Kikwete, ni mimi. Kazi hii haipatikani hivi hivi, naomba dua zenu
Waislamu na Wakristo ni muhimu sana,” alisema Lowassa.
Alisema endapo atafanikiwa kupata nafasi anayoiomba, kwanza atahakikisha anafufua viwanda katika mji wa Morogoro.
Aidha, alisema anasononeshwa mno na migogoro ya wakulima na wafugaji kwa
hiyo atakapoingia madarakani, ataunda tume ya kusuluhisha migogoro
hiyo.
Aliwataka Watanzania wajiandae kuwa na `spidi' ya kuchapa kazi kwani
anataka mchakamchaka wa Maendeleo na atakayeshindwa atalazimika kukaa
pembenBONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI;
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich.
Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music.
She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.
Loading...



Post a Comment