Loading...

HATIMAYE JANUARY MAKAMBA AMTOLEA UVIVU KINGUNGE AAMUA KUSEMA YA MOYONI

BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIUTU UZIMA


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba 
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amemtolea uvivu Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kitendo chake cha kuupinga mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM na kusema anakivuruga chama.


Kingunge aliyejitoa kindakindaki kumpigania mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa jina la Lowassa.


Kamati ya Usalama na Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ndizo zilizokuwa na kazi ya kuchuja majina hadi kupatikana mgombea mmoja, Dk John Magufuli.


Akizungumza jana kwa njia ya simu kutoka Bumbuli Tanga, Makamba (pichani) alisema: “Mzee Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika siasa, lakini anakivuruga chama.”

Alisema binafsi hakubaliani na kauli za Kingunge kupinga uteuzi wa Dk Magufuli kwa sababu makada wote wa chama waliokuwapo Dodoma, waliamua kumpitisha kwa kuwa walimuona anafaa na anaweza kukijenga chama.


“Ndani ya chama kuna wazee wenye busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua mgombea kwani unaweza kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi hivyo, unaweza vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye ushindi.

“Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini siwezi kukubaliana naye anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa sahihi, kila mtu ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa…, tuna imani naye na anaweza kuongoza tangu zamani,” alisema Makamba.


Makamba alisema, ana imani kwamba atafanya vizuri hivyo ni bora apewe ushirikiano kama walivyopewa viongozi waliopita ili kukinusuru Chama cha Mapinduzi na watu waendelee kukiheshimu kama awali.


Kwa upande wa Katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema kwamba, watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli wana masilahi binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho.

Source: Mwananchi
BONYEZA HAPO UONE VIDEO YA MTOTO MKALI; Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWS TIME | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top