Loading...

HUYU NDO MWALIMU ALIYEMPIGA MWANAFUNZI KAMA MWIZI...ANATAFUTWA NA MAWAZIRI WATATU NA POLISI PIA

Huyu ndiye mwalimu Frank Msigwa mtesaji mkuu wa mwanafunzi aitwae Sebastian wa Mbeya sekondari school. Kwa sasa mwalimu huyu ameshafukuzwa chuo na Waziri Ndalichako na anatafutwa na Jeshi la Polisi.

Neno moja kwa mwl. Frank Msigwa.

HIVI NDIVYO RAIS MAGUFULI ALIVYO MWEKA KITIMOTO MTOTO WA DADA YAKE NA KUTAKA KUMTUMBUA MBELE ZA WATU.

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.

Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.

Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.

Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia  gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.

Mtoboa Macho alishinda milioni 20 za Dume Challenge, mshiriki mwenzake amwelezea alivyomfahamu


Wiki hii, habari kubwa nchini ilikuwa ni tukio la mfanyabiashara, Said Ally kutobolewa macho,  usiku katika maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam

Jina la ‘Scorpion’ – mtu aliyefanya unyama huo, limekuwa maarufu pia. Polisi tayari wamemkamata na Jumatano hii alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka mbalimbali yakiwemo kupora na kumjeruhi Said kwa kumchoma visu mwilini na kumtoboa macho yake na kumpa upofu wa ukubwani.
SCORPION NI NANI?

Jina lake halisi ni Salim H Njwete au Samjet. Unaweza ukawa umewahi kumuona sehemu. Mwaka 2012, alikuwa mshindi wa shindano la Dume Challenge lililowakutanisha vijana 20 wababe wa mazoezi na kazi ngumu. Salim alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 20.

Ni mwalimu wa karate na mbabe wa mapigano na ndio maana pindi anamshambulia Said hakuna aliyethubutu kumsaidia kwasababu kila mtu maeneo ya Buguruni anamhofia.

Ni muigizaji wa filamu pia na kwa mujibu wa Walter, aliyekuwa mshiriki mwenzake kwenye Dume Challenge, baada ya mashindano hayo Salim alitoa filamu moja.

Walter ameiambia Bongo5 kuwa Salim alikuwa mtu wa kawaida kabisa na ambaye isingekuwa rahisi kumdhania angekuja kuwa mnyama kiasi hicho.



Walter anasema, Salim ni mjuzi wa mchanganyiko mapigano ya aina nyingi. Anadai aliposikia kuwa ndiye Scorpion, alishangaa mno.

“Lazima nishangae kwasababu, ni kitu ambacho hujawasiliana na mtu kwa muda mrefu kidogo halafu ghafla unakuja kusikia negative side ya mtu ambaye mnafahamiana naye, na ambaye mlishirikiana naye kama wakati tupo kwenye mashindano kule tulikuwa tunalala yaani kitanda hiki hapa na hiki hapa,” Walter ameiambia Bongo5.



“Ni mtu ambaye mmeshirikiana kitu fulani ambacho tayari kilishakuwa on public na watu tayari washajua taswira yenu, sasa mtu anapokuja kufanya kitu kama hicho, ina maana hata wewe mwenyewe unahisi taswira yako inachukuliwa kama vile mshikaji,” ameongeza.

Walter anasema baada ya kushinda milioni 20 kwenye shindano hilo, anachojua ni kuwa Salim aliingia kwenye uigizaji wa filamu na pia alikuwa na mpango wa kwenda kufanya kilimo. Anaeleza kuwa kwenye filamu, Salim alikuwa chini ya Tuesday Kihangala maarufu kama Mr Chuzi.

“Aliamua kuspend hizo hela zake katika movie na akabahatika kutoa movie moja ambayo haikufanya vizuri katika industry,” anaeleza Walter. “Sasa maisha baada ya hapo, sijui ndio akaamua kuspend hela zilizobaki kwenye kitu gani, labda kwenye kilimo kwasababu wakati tulipokuwa naye kule kambini – maake si unajua unamuuliza hizi hela unazifanyia nini, yeye alikuwa amewaza kwenda kulima huko Morogoro.”

Walter amesema  washiriki wenzake wengine wa Dume Challenge wameshangazwa na alichokifanya Salim. “Wako shocked yaani,” anasema. “Ni kitu ambacho hakuna aliyetegemea kwamba jamaa alikuwa anaweza kufanya kitu kama hicho.”

HATIMAYE MBUNGE TUNDU LISSU ASHAMBULIA TELEVISHENI YA TAIFA TBC KWA KUANDIKA UJUMBE HUU MZITO MTANDAONI

https://pbs.twimg.com/profile_images/770991618417692672/_IOom74N_400x400.jpg

Breaking News: Mwamuzi Aliyechezesha Mpira wa Yanga na Simba Afungiwa Miaka Miwili


Habari zilizoifikia ambazo hazijathibishwa na TFF, Bodo ya ligi wala chama cha waamuzi ni kwamba, mwamuzi wa kati Martin Saanya na msaidizi wake namba moja (line one) Samwel Mpenzu, wamefungiwa miaka miwili kuchezesha soka.
Chanzo chetu kimeitutonya kuwa, uamuzi huo umefikiwa na kamati ya saa 72 iliyokutana kuwajadili wawili hao baada ya kuwepo kwa malalamiko kwenye mechi ya Yanga vs Simba waliyoichezesha Jumamosi October 1.
“Martin Saanya na Samwel Mpenzu wamefungiwa miaka miwili lakini line two Ferdinand Chacha yeye amesalimika,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutoandikwa jina.
“Kadi nyekundu aliyooneshwa Jonas Mkude imefutwa baada ya kamai hiyo kujiridhisha kuwa kadi hiyo ilitolewa kimakosa.”
Baada ya mchezo wa Yanga vs Simba, kuliibuka mijadala mingi na mikubwa juu ya mwamuzi Martin Saanya kulikubali goli la Tambwe ambaye aliushika mpira kabla hajafunga huku Samwel Mpenzu akilaumiwa kwa kulikataa goli la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa madai alikuwa ameotea kabla ya kufunga

BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMLIPUA MKE WA WAZIRI LUKUVI KATIKA SHIRIKA LA NDEGE ATCL…HATIMAYE AANDIKA BARUA YA KUJIUZURU


HATIMAYE AFANDE SELE AMTOLEA UVIVU ZITTO KABWE....ASEMA CHAMA CHA ACT WAZALENDO HAKIELEWEKI

Msanii mkongwe wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ambaye alikuwa mgombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka kwa kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Rapper huyo amesema viongozi wa chama chake hawaeleweki wapo upande gani kutokana na kubadilisha misimamo yao kila mara.

“Chama changu cha Act-Wazalendo bwana wakati flani hata mimi sikielewi kama ni malaika au shetani. Ni kama kiumbe aitwae mkunga haeleweki ni samaki au nyoka zaidi tumekuwa kama popo hatupo katika kundi la ndege au mnyama…labda hatueleweki au hatujielewi kwa mfano wakati wa kampeni viongozi wetu walijikita kuponda wapinzani wenzetu hasa mzee Lowasa na UKAWA na baada ya uchaguzi viongozi wetu wakampongeza Magufuli kiasi cha kujipendekeza hadi wakampa Ilani ya chama chetu akaitumie akiwa Ikulu. sasa ajabu leo hii tumegeuka tena kwa kiongozi mkuu kila siku anamponda Rais Magufuli na chama chake halafu kiongozi wangu mwingine comrade mchange yeye kila siku anamponda mzee Lowasa na ukawa yake” aliandika kupitia facebook.

Aliongeza “Katika mgogoro wa CUF unaoendelea sasa hivi eti viongozi wote hao wa chama chetu wamejigeuza team Lipumba…sasa sielewi sisi kama wanachama tusimamie wapi….’Nyuma ya pazia’dilidilisha…mchongo=mchongoma…ni bora kuwa Moto au Baridi kuliko kuwa vuguvugu kwani vuguvugu ni ishara ya unafki ambao hata maandiko yanakataza…Kweli itatuweka huru,”

Tatizo la Nguvu za Kiume....HILI NDILO SULUHISHO NA TIBA SAHIHI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.

Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:

  • Umri wako
  • Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
  • Afya yako kwa ujumla
  • Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
  • Nini sababu ya wewe kutaka kupona
  • Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.


Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake. Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.

Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.

Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke. Sababu nyingine amabzo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;


  • Wasiwasi
  • Hasira
  • Msongo wa mawazo (Stress)
  • Huzuni
  • Hofu na mashaka
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
  • Ili uume usimame vizuri ni lazima:


Mfumo wako wa neva uwe  na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa
Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.


Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:


  • Uzee
  • Kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Kukosa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Ugonjwa wa moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya
  • Kupungua kwa homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
  • Pombe


Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Kitu gani husababisha uume usimame?
Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua  mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.

Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume. Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.

Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.

Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Njia 13 za kujitibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume:

1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.


2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.

Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.
Older Posts
© Copyright NEWS TIME | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top